Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Jenerali wa China, wenzake kuwasili kesho
Jenerali wa China, wenzake kuwasili kesho
By Habari Tanzania | Published  08/18/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Mkolo Kimenya

JENERALI Liu Dongdong wa Jeshi la Ukombozi la Watu wa China (PLA), akiongozana na wajumbe tisa, anatarajia kuwasili kesho kwa ziara ya siku nne.

Jenerali huyo na wenzake, ni wageni wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana ilisema kuwa ziara hiyo ya kirafiki ina lengo la kukuza, na kudumisha uhusiano na ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na China; na kati ya majeshi ya nchi hizo mbili.

Ugeni huo ukiwa nchini, utazuru mikoa ya Arusha na Dar es Salaam, na kuwa na mazungumzo na viongozi mbalimbali. Pia utatembelea vivutio vya utalii.

Ziara hiyo itaanzia Arusha ambako watatembelea maeneo ya utalii ili kujionea utajiri mkubwa wa wanyama.

Baadaye ujumbe huo utakwenda Dar es Salaam ambako kwa nyakati tofauti utakutana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Profesa Juma Kapuya, na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali George Waitara.

Utakamilisha ziara yake kwa kutembelea Makao Makuu ya Kamandi ya Navy, Kigamboni ambako utaonana na Mkuu wa Kamandi hiyo. Pia utazuru Makao Makuu ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA).

Hii ni mara ya nne kwa Tanzania kupokea ujumbe kutoka Jamhuri ya Watu wa China kwa mwaka huu. Ujumbe wa kwanza uliwasili nchini Machi, ukiongozwa na Mkuu wa Mambo ya Nje, Jenerali Zhang Bhandong.

Uhusiano kati ya Tanzania na China ulianza tangu enzi za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere; na Mao Tse Tung.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.