Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mfanyabiashara Dar ajilipua gesti
Mfanyabiashara Dar ajilipua gesti
By Habari Tanzania | Published  08/13/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Mfanyabiashara Mussa Ibrahim Mushi, mkazi wa Tabata, Jijini Dar es Salaam amejiua kwa kujitwanga risasi kichwani akiwa katika nyumba ya kulala wageni Wilaya ya Handeni mkoani Tanga.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Bw. Issaya Mngullu, alisema tukio hilo lililotokea Agosti 10, mwaka huu, katika nyumba ya kulala wageni ya Sawe ya mjini Handeni, ni moja kati ya matukio manne ya mauaji yaliotokea mkoani Tanga hivi karibuni.

Kamanda Mngullu alisema Mushi siku ya tukio, marehemu alipanga chumba namba 25 katika nyumba hiyo ya kulala wageni akitokea Tabata, Jijini Dar es Salaam.

Alisema ilipofika saa 2:00 usiku, mtu huyo aliamua kujiua kwa kujipiga risasi kichwani kwa kutumia bastola aina ya Webley Revolver yenye namba 122122 na kufa pale pale.

Kamanda Mgullu alisema polisi bado hajafahamu chanzo halisi cha mfanyabiashara huyo kujiua na kwamba upelelezi zaidi unaendelea.

Katika tukio lingine, Athumani Juma (8), mkazi wa kijiji cha Kwasingisi, wilayani Handeni, amekufa baada ya kudondoka kutoka ndani ya gari lililokuwa kwenye mwendo mkali.

Kamanda Mngullu alisema baada ya kudondoka, aligongwa na gari hilo lenye namba za usajili T 853 AMH aina ya Toyota Pick up na kufa pale pale.

Alisema tukio hilo lilitokea Agosti 9, mwaka huu katika kijiji cha Kwasingisi.

Katika tukio la tatu, wapanda pikipiki wawili Jimmy Ali Mshiriki (42) na Christina Mwenda (30), wamekufa baada ya kugongwa na gari lenye namba T 654 AET aina ya Escudo.

Tukio hilo lilitokea Agosti 8, mwaka huu eneo la Mizani Nguvumali, mjini hapa ambapo waligongwa wakiwa katika pikipiki namba TZ 99303.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.