Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Bunge lashutumu filamu ya Mapanki
Bunge lashutumu filamu ya Mapanki
By Habari Tanzania | Published  08/12/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Na Martin Malera, Dodoma

SERIKALI imetoa msimamo mzito kwa watumishi na idara zilizohusika na utoaji wa vibali vya kumruhusu Hubert Sauper kuandaa filamu ya Darwin’s Nightmare inayodaiwa kuidhalilisha Tanzania.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Johnson Mwanyika, jana alitangaza azimio la Bunge kuhusu filamu hiyo, inayoeleza minofu huuzwa nje na wananchi kubaki wakila vichwa na mifupa (mapanki), na kutoa karipio kwa mwandaaji Sauper kwa kukiuka miiko ya uandishi wa habari.

Azimo hilo lilitangazwa baada ya Mbunge wa Mchinga, Mudhihir Mudhihir (CCM), kuwasilisha hoja ya dharura kuhusu filamu hiyo na kulitaka Bunge kujadili na kutoa msimamo.

Azimio hilo linasema kulikuwa na uzembe wakati wa utoaji kibali kwani maofisa wa idara husika hawakumfuatilia, na hata alipomaliza kazi yake, hawakutaka kujua picha zilizopigwa.

“Azimio jingine ni kumkaripia mwandishi wa filamu ya Darwins Nightmare kwa kutoa taarifa za uongo, uchonganishi na uzandiki kwa nchi yetu, kwamba biashara ya minofu ya samaki ina uhusiano na uingizaji wa silaha katika nchi za Maziwa Makuu kupitia Jiji la Mwanza isivyo halali,” alisema Mwanyika.

Bunge liliitaka serikali kuweka masharti ya udhibiti wa utengenezaji filamu za aina hiyo, kutengeneza filamu mbadala inayoonyesha upande wa pili wa filamu hiyo ili kusafisha jina la Tanzania, na kutaka serikali ifuatilie ukweli wa tuhuma kwamba ndege zinazotua jijini Mwanza kwa ajili ya kubeba minofu ya samaki, zinaingiza silaha.

Kabla ya kufikia maazimio hayo, wabunge walichangia hoja hiyo. Jackson Makweta wa Njombe Kaskazini (CCM) alivilaumu vyombo vya ulinzi na usalama kwa kumwachia mwandishi huyo aingie nchini na kutengeneza filamu hiyo.

Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo (UDP) alisema: “Mwandishi huyo angekuwa karibu yangu, ningempiga kichwa, amechafua sana jina la Tanzania. Lakini kichwa cha samaki, panki ni mboga nzuri, ikiandaliwa vizuri, ni tamu sana ila serikali iyaweke mapanki katika mazingira mazuri.”

Ester Nyawaza wa Viti Maalumu (CCM), alisema ukahaba unaoonyeshwa katika filamu hiyo ni kawaida na si tatizo la Mwanza pekee.

Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Omar Yusuph Mzee, alilaani kitendo cha watoto kutumika kwenye filamu hiyo kuonyesha umaskini wa Watanzania na wanawake walioonyeshwa kwenye mambo ya ukahaba.

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), alisema filamu hiyo ina athari kubwa kwa biashara ya samaki katika Ziwa Victoria, akafadhaishwa na Waziri Mkuu, Edward Lowassa kujadili suala hilo na wabunge wa CCM, na kuwaacha wabunge wa upinzani wakati ni la maslahi kwa taifa.

Kabwe aliwalaumu mawaziri kwa kumwachia Rais Jakaya Kikwete kutangaza ubaya wa filamu hiyo, akawataka wawe makini muda wote.

Mbunge wa Bumbuli, William Shelukindo (CCM) alisema mapanki yakiwekwa kwenye mazingira mazuri ni chakula kitamu, hivyo aliitaka serikali ihakikishe mazingira hayachafuliwi. Alimfananisha Sauper na gaidi.

Rais Jakaya Kikwete, Julai 31 akizungumza na wazee wa Mwanza, ndiye aliyeanza kusema filamu hiyo ni ya uongo na uzandiki.

Wakati huo huo, Spika wa Bunge, Samuel Sitta amekikemea Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuacha vikao vya faragha yanapojitokeza masuala yanayohitaji mjadala wa kitaifa.

Hali hiyo ilijitokeza baada ya kambi ya upinzani bungeni kukosoa wabunge wa CCM waliokutana kwa faragha kujadili suala la filamu ya Darwin’s Nightmare na kisha kuwasilisha hoja hiyo bungeni kwa ajili ya kutolewa azimio la pamoja la Bunge.

Juzi, Waziri Mkuu, Edward Lowassa, baada ya kipindi cha maswali na majibu kumalizika, aliongoza kikao cha faragha cha wabunge wa CCM, kujadili suala la filamu hiyo inayodaiwa kuchafua jina la Tanzania kutokana na maudhui yake.

Spika alitoa kauli hiyo akijibu baadhi ya wabunge wa kambi ya upinzani ambao wakati wa kuchangia hoja ya filamu hiyo, walianza kukosoa tabia ya wabunge wa CCM kuendeleza vikao vya faragha hata katika masuala ya kitaifa ambayo yanahitaji umoja bila kujali itikadi.

Mbunge wa Gando, Khalifa Suleiman Khalifa (CUF) ambaye ni Chief Whip na Msemaji Mkuu wa Upinzani kwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ndiye aliyekuwa wa kwanza kutoa lawama hizo dhidi ya wabunge wa CCM.

Mbunge huyo alimueleza Spika kuwa wapinzani licha ya uchache wao bungeni, wana haki ya kushiriki katika mijadala ya mambo yanayohusu taifa na azimio lililopendekezwa na Mbunge wa Mchinga, Mudhihir Mudhihir dhidi ya filamu ya Darwin’s Nightmare ni la upande mmoja na kutaka lijumuishe vyama vyote.

Kauli hiyo iliungwa mkono na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Ztito Kabwe (CHADEMA) na Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo (UDP), ambao walisisitiza kuwa upinzani unatambulika katika katiba ya nchi na uzito wake kwa upande wa maoni ni sawa na wabunge wa CCM bila kutanguliza suala la idadi ya wabunge.

Hata hivyo, wabunge wa CCM akiwamo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Benard Membe, walipingana na hoja hizo za wabunge wa upinzani, wakisema vikao vya faragha kwa wabunge wa CCM ni jambo lisiloepukika na si jambo jipya kwa mabunge duniani na kutoa mfano wa Bunge la Canada.

Kutokana na hali hiyo, Spika Sitta, alilazimika kusawazisha mambo akisema katika masuala yote yanayohusu maslahi ya taifa, hata kama wabunge wa CCM wakiwa wamekutana kwa faragha, si vibaya kujadili na wabunge wa upinzani kabla ya kuingia bungeni ili kuwa na msimamo unaoeleweka katika masuala ya kitaifa.

Kumekuwapo na tabia inayoendelea kukomaa bungeni, hususan yanapojitokeza masuala ya kitaifa, CCM imekuwa ikijitenga na kuendesha vikao vya faragha kwa kutumia wingi wa idadi ya wabunge wake.

Siku ya Nanenane mara baada ya wabunge kuonyeshwa filamu ya Darwin’s Nightmare, Waziri Lowassa, aliwatangaziwa wabunge wa CCM kukutana faragha kujadili suala hilo, siku iliyofuata


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.