Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Maofisa usalama bandia Z’bar
Maofisa usalama bandia Z’bar
By Habari Tanzania | Published  08/11/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

WATU wawili wamekamatwa visiwani hapa, wakifanya utapeli na kujipatia sh milioni 2.5, wakati walipojifanya maofisa usalama wa taifa, waliopewa kazi maalumu na Rais Jakaya Kikwete.

Watu hao; Khatim Mohammed Khatib (30) mkazi wa Magomeni mjini Unguja na Mohammed Mutalia (46) wa Fuoni, Wilaya ya Magharibi Zanzibar, walikamatwa baada ya kumtapeli Ali Hassan Rajab, wakimweleza ni wajumbe wa Tume Maalumu ya Usalama wa Taifa iliyoundwa na Rais Kikwete.

Baada ya polisi kuwakamata, walifikishwa Mahakama ya Mwanakwerekwe, mbele ya Hakimu Janet Sekihola, na kusomewa mashitaka ya kujipatia kima hicho cha fedha kwa njia ya udanganyifu.

Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Haji Abdallah, alidai mahakamani hapo kuwa, washitakiwa walitenda kosa hilo eneo la Kibandamaiti Julai 31, majira ya saa 3:30 asubuhi.

Alidai kwamba watuhumiwa walifanikiwa kuchukua fedha, baada ya kujitambulisha kuwa ni maofisa wa tume hiyo maalumu, na wanahitaji kiasi hicho cha fedha.

Washitakiwa hao walikana mashitaka na Hakimu Sekihola aliwataka waandikishe dhamana ya maandishi ya sh milioni moja na mdhamini mmoja mwenye kitambulisho. Kesi hiyo itatajwa tena mahakamani hapo Agosti 21, mwaka huu na watuhumiwa wako nje.

Wakati huo huo, askari wa Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar (JKU), Ali Shaha Ali (29), amefikishwa mahakamani, akituhumiwa kujihusisha na vitendo vya ujambazi. Askari huyo anatoka Makao Makuu ya JKU, Saateni mjini Unguja.

Ilidaiwa mahakamani na mwendesha mashitaka, Fatma Abdallah Hassan kuwa, askari huyo na wenzake walifanya shambulio la kumvamia mfanyabiashara Mohammed Nassor Suleiman Msumar na kuiba mali inayokisiwa kufikia sh milioni 20.5 mnamo Julai 4, mwaka huu, katika mtaa wa kibiashara wa Darajani


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.