Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  RAIS AENDA MKOANI MARA KWA ZIARA YA SIKU SITA
RAIS AENDA MKOANI MARA KWA ZIARA YA SIKU SITA
By Habari Tanzania | Published  08/8/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:
Rais Jakaya Kikwete kesho anaanza ziara ya kikazi ya siku sita Mkoani Mara.
 
Akiwa Mkoani humo, Rais atazindua miradi mbalimbali ya maendeleo, kuhimiza shughuli za maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi katika mikutano ya hadhara.
 
Miradi ambayo Rais ataifungua ni wadi ya watoto na wazazi katika Hospitali ya Mkoa, kutembelea na kukagua shule ya Sekondari Bulhmba na kukagua shughuli za ukulima wa kisasa.
 
Aidha Rais akiwa mkoani humo, pia atakwenda wilaya ya Bunda ambako ataweka jiwe la msingi la Hospitali ya Wilaya na kufanya mkutano wa hadhara.
 
Baada ya kutembelea wilaya ya Bunda, Rais atakwenda wilaya ya Tarime ambako atakagua miradi ya ufugaji, kilimo na zahanati, kufungua shule ya Sekondari ya Bukama, na kuzindua jengo la Halmashauri na kuhutubia mkutano wa hadhara.
 
Rais pia atatembelea wilaya ya Serengeti ambako atafungua bweni la wasichana katika shule ya Sekondari ya Natta na kuhutubia mkutano wa hadhara.
 
Rais atarejea jijini Dar es Salaam Agosti 14.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.