Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mihadhara ya dini Kigogo ikemewe
Mihadhara ya dini Kigogo ikemewe
By Habari Tanzania | Published  08/6/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated

WAKAZI wa Kigogo, jijini Dar es Salaam, wamekuwa wakikerwa na jambo hili kwa muda mrefu.


Lakini mwishowe wamekerwa na uzembe wa serikali ambayo wanaiona imeshindwa kuchukua hatua dhidi ya watu wanaoendesha mihadhara ya kidini kila jioni katika nafasi ya wazi, pembeni mwa barabara itokayo Kigogo kuelekea Mburahati.


Wahubiri wa dini za Kiislamu na Kikristo, wametumia vibaya uhuru walionao kuhubiri imani yao. Badala yake sasa, wanatumia vema uzembe wa serikali kuwatukana na kuwakashifu waamini wa dini nyingine. Wakristo wanawabeza Waislamu, na Waislamu wanawabeza Wakristo.


Inavyoonekana, wanapeana muda; kwani siku ya mhadhara wa Kikristo, Waislamu hawawi na mhadhara. Na siku Waislamu wanapokuwa na mhadhara wao, Wakristo hawawi na mhadhara.


Katika hali ya kawaida, ni rahisi kudhani kwamba watu hawa wanapanga, na kupeana nafasi ya kuchuma pesa, kwani kila baada ya mikutano yao hutangaza maombi ya michango kwa ajili ya vipaza sauti, mafuta na kadhalika.


Wengi wanaohudhuria mihadhara hiyo ni vijana. Mihadhara yenyewe haina nia ya kujenga imani za wasikilizaji. Vile vile, haionekani kama inaendeshwa na watu waadilifu, kwani muda mwingi wanautumia kuwakashifu wenzao.


Kibaya zaidi ni kwamba Wakristo wanatumia muda mrefu kuzungumzia ubaya wa Uislamu, huku wakinukuu zaidi Kurani kuliko Biblia. Waislamu nao vile vile; wanatumia Biblia kuukosoa na kuukashifu Ukristo na kusababisha vicheko vya kebehi kutoka kwa wasikilizaji.


Hawa hawahubiri uongofu wala wokovu wa kiimani. Hatima ya mahubiri haya, ni dharau, chuki na ugomvi miongoni mwa waamini wanaoshutumiana.


Zaidi ya hayo, mihadhara hii hufanyika usiku, si mchana. Hufanyika muda ambao hauruhusiwi kwa mikutano ya hadhara kwa sheria za nchi.


Kwa sababu hizo, serikali iliwahi kupiga marufuku mihadhara hii ya dini. Kwa muda, ilipotea. Lakini sasa imeanza, wahubiri hawa wamerudi kwa ubabe na dharau kubwa dhidi ya serikali.


Nasi tunashangaa kwamba serikali inayojitapa kuongoza nchi ya amani, inaacha mizizi ya amani inag’olewa. Serikali inakubali kulala usingizi wa pono! Tunatoa wito, serikali iamke, ikemee mihadhara hii, iwashughulikie wahubiri hawa.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.