Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Polisi watatu mbaroni kwa mauaji ya kijana
Polisi watatu mbaroni kwa mauaji ya kijana
By Habari Tanzania | Published  08/4/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Polisi watatu mbaroni kwa mauaji ya kijana
 
Na Mkami Shanyangi, Manyara
 
ASKARI watatu wa Jeshi la Polisi na wananchi wawili wilayani Babati, mkoani hapa, wametiwa mbaroni kwa tuhuma za mauaji.
 
Wanashikiliwa katika Kituo cha Polisi mjini hapa, wakituhumiwa kumpiga hadi kumuua mfanyabiashara, Mihayo Manyika (20). Polisi wanadai kwamba, kijana huyo alimrubuni mwanafunzi mwenye umri wa miaka 15 kwa kumnywesha pombe ili afanye naye mapenzi.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Neven Mashayo, aliwataja askari hao kuwa ni PC Tumaini Mwenye namba F 5073, ambaye ndiye kiongozi; PC Judica D 9664 na PC Rashid E 4674.
 
Wengine ni wananchi wawili ambapo mmoja ni baba mzazi wa mwanafunzi huyo na rafiki wa marehemu huyo Patrick Joel (20), maarufu kwa jina la Mwenge.
 
Baba wa marehemu, Paulo Mihayo, akijieleza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Kanali Anatoli Tarimo na Kamanda Mashayo, alisema askari hao wanahusika katika tuhuma hizo, kwa madai kuwa walikodiwa na baba mzazi wa mwanafunzi huyo kumdhuru.
 
Mzazi huyo alitoa malalamiko hayo huku akiungwa mkono na ndugu na wananchi wenye hasira walioandamana na kuvamia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, wakitaka atoe tamko juu ya utendaji mbovu wa polisi mkoani hapa.
 
Katika malalamiko yao, baba wa marehemu alidai kuwa tangu tukio hilo lilipotokea Agosti 1, 2006 majira ya saa 2 usiku, polisi walikuwa wakiwapiga danadana na kushindwa kuwafungulia jalada la mashtaka askari waliompiga mwanawe, huku askari hao watatu wakirandaranda mitaani, hadi mwanawe alipokata roho.
 
Kamanda Mashayo alisema Manyika alimnywesha mwanafunzi huyo katika baa ya Madiven mjini hapa, kabla ya mzazi wa mwanafunzi huyo kuwafumania na kumpiga kijana huyo na rafiki yake.
 
Baadaye askari hao walitokea, wakatuliza ghasia, kisha wakampiga kijana huyo na kumjeruhi vibaya, akapoteza fahamu, kisha akafariki dunia.
 
Mji wa Babati ulibadilika kwa muda, kutokana na maandamano na jinsi wananchi walivyoonyesha kuwa na hasira, kutokana na polisi hao kuua, ikiaminika kwamba walikodiwa.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.