Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Ngoma nzito madaktari, serikali
Ngoma nzito madaktari, serikali
By Habari Tanzania | Published  08/4/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Ngoma nzito madaktari, serikali
 
Grace Hilly (SAUT) na Magreth Kinabo
 
WIZARA ya Afya na Ustawi wa Jamii, imeitisha kikao kati ya maofisa wake na madaktari bingwa ambao hawaridhishwi na kufutwa cheo hicho.
 
Kuanzia jana asubuhi hadi alasiri, maofisa wa wizara walikuwa wanakutana na wawakilishi wa madaktari hao, wanaohoji sababu za kufutwa cheo hicho kinachopatikana baada ya kusota darasani kwa miaka mitatu, wakibobea kwenye eneo maalum kimatibabu.
 
Wizara katika uamuzi wake, iliwatupa madaktari hao kwenye kapu la madaktari waandamizi, ambamo wapo hata wasiosota darasani, ilimradi tu umepita muda mrefu wakiwa kazini. Kipato pia kinapungua kwa kuondoa cheo hicho.
 
Akizungumza na Tanzania Daima katika ofisi za Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Mchembe Mabula, alisema bado hawajapata ufafanuzi kutoka wizarani.
 
"Leo (jana) nimepata taarifa kuwa watu wa wizarani wamekuja kuzungumza na madaktari bingwa, hivi sasa bado wanaendelea na kikao.
 
“Kwa sasa mimi siwezi kusema lolote, tunasubiri ufafanuzi wa kina kutoka kwa wizara baada ya kikao kuisha, ili tupate uhakika wa suala hili kwa vile wizara ilitoa tamko bila kutupa taarifa wote, hatimaye na sisi tujue cha kufanya,” alisema.
 
Alisema wataendelea kulishughulikia suala hilo, hadi watakapofikia muafaka na wizara.
 
“Kwa leo (jana) si rahisi kuzungumza zaidi, maana sijui kinachoendelea kwenye kikao hicho. Hapa nilipo naenda kwenye kikao kingine tofauti hadi hapo kesho nitakapopata taarifa za kikao hicho,” alisema Dk. Mabula.
 
Katika barua yake ya Januari 17, mwaka huu, kwenda kwa mmoja wa madaktari bingwa waliohitimu, aliyekuwa akitaka apandishwe cheo, ilieleza bayana kwamba cheo hicho kimefutwa.
 
Kabla ya ya mabadiliko hayo, daktari mwenye digrii ya kwanza, alikuwa anasoma digrii ya uzamili (clinical) kwa mika mitatu, kisha anatambulika kama daktari bingwa, halafu anapandishwa ngazi tatu za mshahara.
 
Lakini baada ya mabadiliko hayo, daktari huyo haitwi daktari bingwa, bali anaitwa daktari mwandamizi, cheo ambacho hata mtu ambaye hakusoma shahada ya uzamili ya miaka mitatu hukipata kwa kukaa muda mrefu kazini.
 

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.