Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  JK kuhutubia Taifa leo akizungumza na wazee Mwanza
JK kuhutubia Taifa leo akizungumza na wazee Mwanza
By Habari Tanzania | Published  07/31/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:
Rais Jakaya Kikwete, leo atalihutubia Taifa kwa kuzungumza na Wazee wa Mkoa wa Mwanza.

Mazungumzo kati ya Rais na Wazee hao, yatafanyika saa 10:00 jioni katika ukumbi wa Chuo cha Benki Kuu (BoT), Jijini Mwanza.

Taarifa ya Ikulu Jijini Dar es Salaam ilisema, hotuba hiyo ni mwendelezo wa utaratibu wake aliojiwekea wa kuzungumza na wananchi kila mwisho wa mwezi.

Taarifa ilifafanua kuwa, mazungumzo hayo yatarushwa moja kwa moja na kituo cha Televisheni cha Star TV na Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD).

Katika hatua nyingine, akiwa mkoani Mwanza, Rais atakitumia kipindi cha kuanzia Agosti Mosi hadi 6, mwaka huu kwa mapumziko mafupi.

Taarifa ilifafanua kuwa, pamoja na kuwa katika mapumziko, Rais atakuwa na ratiba nyepesi ya kutembelea Kiwanda cha Kusindika Minofu ya Samaki na Kiwanda cha Nguo cha Mwatex.

Ilisema Agosti 7, mwaka huu, Rais ataondoka mkoani Mwanza na kwenda mkoani Arusha ambako siku inayofuata, atakuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya Wakulima yaani Nane Nane.

Ilifafanua kwamba, kuanzia Agosti 9, mwaka huu, Rais Kikwete ataanza ziara ya kikazi mkoani Mara kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.