Rais Jakaya Kikwete, amewateua Wakuu wa Wilaya wapya 46, kuwafuta kazi 13, wengine 17 wamestaafishwa kutokana na umri na 58 wamebadilishwa vituo vyao vya kazi.
Katika uteuzi huo, wengi ni wanawake wakiwemo waandishi wa habari Bi. Betty Mkwassa, mtangazaji wa zamani wa ITV, Bi. Sarah Dumba, mtangazaji wa Radio Tanzania (RTD) na Bw. Abihud Saideya, aliyekuwa mwandishi wa habari wa magazeti ya Uhuru na Mzalendo.
Hatua ya uteuzi wa wanawake wengi inaonekana ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa na Rais Kikwete wakati wa kampeni za uchaguzi muu ya kuhakikisha kwamba wanawake wanapewa nafasi nyingi za juu za uongozi serikali.
Taarifa ya Ofisi ya Waziri Mkuu mjini Dodoma jana iliwataja Wakuu wa Wilaya wapya walioteuliwa na vituo vyao kwenye mabano kuwa ni, Deodatus Kinawiro (Mkinga), Kanali Edmund Mjengwa (Shinyanga) Dk. Charles J. Tzeba (Sikonge), Anna Magowa (Liwale), Mathew Kanjalo Nasei (Magu), Elinas A. Pallangyo (Sengerema), Hawa Ngh’umbi (Mvomero), Anna Nyamubi (Siha) Danhi Makanga (Kwimba), John Henjewele (Kiteto), Chiku Galawa (Bunda) na Gishuli Mbegesi Charles (Mtwara).
Wengine wapya ni Lephy Gembe (Makete), Reuben N. Shigela (Lindi), Dk. Evarist Ndikilo (Kilombero), Stanley Kolimba (Tarime), Patrick Tsere (Ilala), Betty Mkwasa (Korogwe), Luteni Edward Ole Lenga (Serengeti), Thobias Manzala (Mpanda), Kanali F. T. Massawe (Kinondoni) na Lembris Kipuyo (Kongwa).
Wakuu wa Wilaya wapya wengine ni Mariam L. Sefu (Rungwe), Sevell Maketta (Musoma), John Mongela (Kigoma), Rashid Ndaile ((Nachingwea), Manzie Mangochie (Mafia), Zipora Pangani (Pangani), Nurdin Babu (Kilwa), Dk. Ramadhani Lutengwe (Ulanga), Abihud Saideya (Meatu) na Said Ali Amanzi (Masasi).
Wengine wapya ni Hasna Mwilima (Hai), Ibrahim W. Marwa (Same), Francis C. Miti (Tandahimba), Jackson Msome (Newala), Athumani Mfutakamba (Kilolo) Dk. Betty Machangu (Nzega), Kassim Majaliwa (Urambo), Sarah Dumba (Kilindi), Saidi Bwanamdogo (Kasulu), Khalid Mandia (Simanjiro), Sofia Mjema (Lushoto), Doreen Kisamo (Uyui), Halima Dendego (Mpwapa) na Georgina Elias Bundala (Ludewa).
Wakuu wa Wilaya waliostaafishwa kutoka na umri wao na vituo walivyokuwa wanafanyia kazi kwenye mabano ni, Fulgence Lucas Saria (Arusha), Kapteni Anthony Malley (Monduli), Pascal T. Mhongole (Mufindi), Bernad Maduhu Itendele (Kilwa), Alhaj Ahmed Lugusha (Bukoba) ACP Simon Massaga (Misungwi), Miraji H. Pazi (Meatu), Pastori Kazi Mwibule (Sikonge) na Dk. Deogratias Mwita (Kilombero).
Wengine waliostaafishwa ni Kanali Laban Makunenge (Kasulu), David J. Daud (Karagwe), Jaffer K. B. Mpili (Rufiji), Luteni Shaaban Muyombo (Dodoma), Osmund Kapinga (Makete), Luteni Baltazari K. Minja (Kilolo), Mansueta Sanka (Shinyanga) na Brigedia Jenerali Sylivester Hemed (Ulanga).
Wakuu wa Wilaya waliotemwa katika uteuzi huo ni, Bertha Mende (Rungwe), Esther Malyeta (Sengerema), Jared Ghachocha (Ilemela), Ernest Daudi Masima (Manyoni), Andrea J. Masanje (Kahama), Luteni Lepilal Ole Molloimet (Kiteto), Mark Daffa (Nachingwea), Aloyce E. Komba (Hai), Edward M. Maleyek (Kishapu), Tatu Ibrahim Ruta (Iringa), Ferdinand B. Mkude (Same), Ali Mohammed Libaba (Mafia) na Severine Mhuwa (Kwimba).
Wakuu wa Wilaya waliobadilishwa vituo vya kazi ni:- Kapteni Aseri G.N. Msangi (kutoka Ngorongoro kwenda Nanyumbu), Baraka Mbike Konisaga (kutoka Temeke kwenda Bariadi), Athuman Mdoe (kutoka Kinondoni kwenda Kilosa), Amina J. Masenza (kutoka Kondoa kwenda Mbinga), Ali Nassoro Rufunga (kutoka Masasi kwenda Rufiji), Zainab Kondo (kutoka Iramba kwenda Muheza), Dk. Ian J. Langiboli (kutoka Mpanda kwenda Chamwino), Joyce Wangan Kingu (kutoka Muheza kwenda Nkasi), Thomas Ole Sabaya (kutoka Serengeti kwenda Songea), Abdallah Ali Kihato (kutoka Karatu kwenda Temeke), Kapteni Godfrey P. Ngatuni (kutoka Tanga kwenda Hanang), Moshi Mussa Chang’a (kutoka Mbeya kwenda Tabora), Luteni Kanali S. M. Mrengo (kutoka Biharamulo kwenda Bagamoyo), Peter Toima Kiroya (kutoka Nyamagana kwenda Ukerewe), Cleophas Angelo Rugarabamu (kutoka Bariadi kwenda Igunga), Saidi Mkoma Mkumbo (kutoka Nkasi kwenda Chato) na Ernest N. Kahindi (kutoka Musoma kwenda Biharamulo).
Wakuu wa Wilaya wengine waliobadilishwa vituo vya kazi ni Pascal Mabiti (kutoka Tarime kwenda Manyoni), Henry Orauya Clemence (kutoka Kigoma kwenda Mkuranga), Elias Kajeli Maarugu (kutoka Magu kwenda Misenyi), Kanali Peter Madaha (kutoka Uyui kwenda Nyamagana), Mussa Hilal Samizi (kutoka Tabora kwenda Moshi), Elaston Mbwilo (kutoka Mbinga kwenda Iringa), Kapteni James Yamungu (kutoka Singida kwenda Maswa), Jowika Wilson Kasunga (kutoka Maswa kwenda Ngorongoro), Evans Balama (kutoka Sumbawanga kwenda Arusha), David W.A. Holela (kutoka Liwale kwenda Babati), Grace Mesaki (kutoka Kisarawe kwenda Iramba), Elias Goroi (kutoka Lushoto kwenda Mbulu), Leonidas T. Gama (kutoka Newala kwenda Mbeya), Mashimba H. Mashimba (kutoka Mbulu kwenda Kyela), Evarist N. Kalalu (kutoka Kyela kwenda Mufindi) na Mathew Saria Sedoyeka (kutoka Morogoro kwenda Karatu).
Wengine waliohamishwa ni Luteni Kanali Issa Salehe Machibya (kutoka Kilosa kwenda Monduli), Abeid Mwinyimusa (kutoka Songea kwenda Bukoba), Kapteni Seif A. Mpembenwe (kutoka Ilala kwenda Kondoa), Hawa Mchopa (kutoka Igunga kwenda Rwangwa), Meja Bahati Matala (kutoka Urambo kwenda Sumbawnga), Luteni Winfrid Francis Ligubi (kutoka Kilindi kwenda Handeni), Khanifa M. Karamagi (kutoka Mkuranga kwenda Kisarawe), Ibrahim Msengi (kutoka Babati kwenda Tanga), Philemon M. Shelutete (kutoka Simanjiro kwenda Geita) Fatuma L. Kimario (kutoka Tandahimba kwenda Chunya), Frank A. A. Uhahula (kutoka Chunya kwenda Karagwe), Khadija Nyembo (kutoka Ukerewe kwenda Kishapu), Florence A. Horombe (kutoka Kongwa kwenda Singida), Magalula S. Magalula (kutoka Pangani kwenda Misungwi), Kanali Salum W. Nyakonji (kutoka Korogwe kwenda Ngara), Hawa Ngulume (kutoka Bagamoyo kwenda Mbarali), James K. Ole Millia (kutoka Moshi kwenda Longido), Halima Meza Kihemba (kutoka Njombe kwenda Mbozi), Darry I. Rwegasira (kutoka Mbozi kwenda Njombe), John J. Tuppa (kutoka Muleba kwenda Dodoma M.), Deusdedit Mtambalike (kutoka Ludewa kwenda Muleba), Gilbert Dololo (kutoka Mbarali kwenda Kibaha), Kanali Kelvin Msemwa (kutoka Hanang kwenda Kahama) Said T. Mwambungu (kutoka Kibaha kwenda Morogoro) na Samwel Kamote (kutoka Mvomero kwenda Ilemela).
Wakuu wa Wilaya wanaobaki katika vituo vyao ni Elias Wawa Lali (Arumeru), Zainab Kikwega (Bahi), Raymond H. Mushi (Rombo), Jordan M. O. Rugimbana (Mwanga), Ester Philipo Wakari (Ileje), Albert Mnali (Tunduru), Gabriel Gwabi Kimolo (Namtumbo), Paul V. J. Chiwile (Bukombe) na Luteni Kanali John A. Mzurikwao (Kibondo).
Taarifa hiyo ilisema Rais Kikwete amewaagiza Wakuu wa Mikoa kuwaapisha Wakuu wa Wilaya wote kabla ya Ijumaa, Agosti 4, mwaka huu.