Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Machinga Dar yametimia
Machinga Dar yametimia
By Habari Tanzania | Published  07/28/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated

Na Magnus Mahenge

RAIS Jakaya Kikwete amewataka Wamachinga waliozagaa mitaani na barabarani Dar es Salaam, kuhamishia biashara na shughuli zao kwenye masoko yaliyotengwa na Jiji kwa ajili ya shughuli hizo.

Rais alitoa amri hiyo jana wakati akizungumza na wafanyabiashara wa soko la Mchikichini, Ilala, Dar es Salaam, katika siku ya kwanza ya ziara yake ya siku tatu mkoani humo.

Kauli hiyo ilikuwa ni majibu ya kilio cha baadhi ya Wamachinga wanaoendesha biashara zao sokoni hapo, ambao walimlalamikia kuwa biashara zao zimedoda kutokana na ukweli kwamba miongoni mwao wamerudi kufanya biashara mitaani, barabarani, kwenye njia za waenda kwa miguu na mbele ya maduka ya watu, Kariakoo.

Aliwataka Wamachinga hao wahame mara moja na akaahidi kuwa muda waliopewa wa miezi sita, ambao unaokwisha mwezi ujao, wawe wamehamisha shughuli zao kwa ustaarabu.

Alisema Serikali haiwezi kufumba macho wakati inaona Wamachinga wamegeuza kila mahali mitaani, barabarani na kwenye njia za kupita watu kwa miguu panakuwa mahali pa biashara, kama ikifanya hivyo itakuwa Serikali ya ajabu isiyozingatia utaratibu na sheria zake.

Alikumbusha kuwa, amri iliyotolewa na Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa ya kusimamisha bomoabomoa jijini katika kipindi cha miezi sita, ililenga kuwapa nafasi Wamachinga kuhamisha shughuli zao badala ya Jiji kutumia tingatinga kubomoa, badala yake wamekuwa hawahami na wengine wanarudi mitaani, barabarani na mbele ya maduka ya wengine.

"Hakuna atakayewakingia kifua baada ya muda huo kwisha na wale wote watakaopuuza watapambana na askari wa Jiji ambao watafanya kazi hiyo, lakini mnaijua kazi ya askari hao," alisema.

Rais aliahidi kuwapa kipaumbele wanaoendesha shughuli zao sokoni hapo kihalali na akaahidi kuwa sh. milioni 500 zilizotolewa na Serikali, watapewa kipaumbele.

Kuhusu nyumba 276 za Ilala zilizochakaa, aliitaka Manispaa ya Ilala kuzibomoa, lakini akaagiza mara nyumba bora zitakapojengwa, waliokuwa wakazi wake ndio wapewe kipaumbele.

Katika ziara hiyo wilayani Ilala, Rais pia alitembelea kiwanda cha nguo cha Lamkan akawataka wamiliki wake kutumia teknolojia mpya na mashine za kisasa, ili kupata faida na tija na kuachana na mtindo wa kuagiza malighafi China na India, wakati zinapatikana nchini.

Mapema Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Abbas Kandoro, alisoma taarifa ya maendeleo ya mkoa, ambapo pamoja na mambo mengine mkoa uliishukuru Serikali kwa kutoa sh. milioni 500 kila mkoa lakini wakaomba kuongezwa fedha hizo.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.