Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mbrazili wa Stars atua na kunena...Watanzania msitarajie miujiza
Mbrazili wa Stars atua na kunena...Watanzania msitarajie miujiza
By Habari Tanzania | Published  07/27/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated

Na Abdallah Mweri

KOCHA Mkuu mpya wa timu ya soka ya Taifa (Taifa Stars), Marcio Maximo wa Brazili, amewasili nchini na kusema Tanzania isitarajie miujiza kushiriki michuano ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika Ghana mwaka 2008.

Maximo aliwasili kwenye Uwanja Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam jana saa 8.20 mchana kwa ndege ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini akitokea Brazili, akiwa ameongozana na kocha msaidizi wa timu hiyo kwa ajili ya mazoezi ya viungo, Itamar Amorion ambaye pia ni raia wa Brazili.

Kocha huyo alilakiwa na baadhi ya viongozi wa Serikali wakiongozwa na Mkurugenzi wa Michezo wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Henry Ramadhani.

Akizungumza uwanjani hapo, Maximo alisema Tanzania isitarajie kushiriki fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika Ghana kutokana na muda mfupi alionao kabla ya mechi za kuwania kufuzu ambapo imepangwa kuanza na Bukinafaso Septemba, mwaka huu.

Mbali na Bukinafaso, Tanzania imepangwa kundi la saba pamoja na Senegali na Msumbiji. Kila kundi linatoa timu moja inayofuzu fainali hizo.

Maximo alisema mpira si hesabu ya sayansi, unahitaji mambo mengi ikiwa ni pamoja na maandalizi ya kutosha kutoka kwa vyama husika, wachezaji na wadau mbalimbali wa mchezo huo.

"Nina matumaini makubwa na Tanzania ingawa ni mara yangu ya kwanza kufundisha timu za Afrika lakini hilo sina shaka nalo kwa kuwa nimewahi kuwafunisha wachezaji wengi wanaotoka huku na pia katika nafasi yangu ya ukocha nimewahi kukutana na timu za Afrika," alisema kocha huyo.

Maximo aliyeonekana mcheshi muda wote wakati akizungumza na waandishi wa habari, alisema anajua Watanzania wana kiu kubwa ya kuona timu yao inashiriki fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika hivyo atajitahidi kadri ya uwezo wake kuhakikisha inaibuka mshindi kundi lake na kupata tiketi ya kucheza fainali hizo.

Alisema kwa kushirikiana na viongozi wa TFF, atawashauri kutengeneza programu kwa ajili ya kuunda timu za vijana wadogo wa rika mbalimbali ambao ndio msingi mkuu wa kukuza kiwango cha mchezo huo duniani.

"Mpira si kama paa la nyumba kwamba siku zote linakuwa juu tu, soka inaanza chini hivyo ni vyema watu wakatambua hilo ili mchezo huu upige hatua kama zilivyo nchi zilizoendelea duniani ni lazima utengenezwe msingi kwanza kwa kuchagua vijana wadogo ambao baadaye watakuwa hazina kwa timu zetu za Taifa," alisisitiza Maximo.

Alisema Afrika inaundwa na wachezaji wengi wenye vipaji vya kucheza sehemu yoyote duniani na Tanzania ni miongoni mwa nchi hizo, hivyo cha msingi iandaliwe mikakati madhubuti inayoweza kuinua kiwango cha mchezo huo ikiwa ni pamoja na kuandaa timu nyingi za vijana wadogo.

Maximmo ana shahada ya juu ya ufundishaji wa soka aliyoipata mwaka 1992 Chuo Kikuu cha Federal do Rio De Janeiro (UFRJ). Aliwahi kuzifundisha timu za taifa za vijana wenye umri chini ya miaka 17 na 20 na mwaka 1994 aliwahi kuifundisha timu ya taifa ya Katari iliyofuzu mashindano ya kuwania ubingwa wa Asia.

Nchi nyingine alizowahi kufundisha ni timu ya taifa ya vijana wenye umri wa miaka 20 ya Indonesia, timu ya Al Ahli Club ya Jeddah Saudia mwaka 1995 na timu ya Livingstone FC ya Skotilandi mwaka 2003/2004.

Ciao...


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.