Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mpasuko wa kisiasa Z'bar wawa mwiba
Mpasuko wa kisiasa Z'bar wawa mwiba
By Habari Tanzania | Published  07/27/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated

*Alipelekwa kwa mganga huyo kutibiwa uzazi
Na Gurian Adolf, Sumbawanga
MGANGA wa jadi, Bw. Peter Kapondo (28), alimeuawa kwa kipigo kutokana na tuhuma za kufanya mapenzi na mke wa mtu.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, Bw. Germanus Mponguliana, alisema tukio hilo litokea Julai 20 mwaka huu.

Alisema kabla mauaji hayo wanandoa, Bw. Romadi Kalipesa (43) na mkewe (jina linahifadhiwa) walikwenda kwa mganga huyo kwa lengo mwanamke huyo kutibiwa matatizo ya uzazi ambayo yamemfanya kuishi muda mrefu bila kupata mtoto.

Wakati wakiwa kwa mganga huyo, Kamanda alisema wanandoa hao waliambiwa na mganga kuwa ili mwanamke huyo aondokane na matatizo hayo, ilibidi mumewe amwache kwa mganga ili akafanyiwe matambiko usiku.

Bw. Kalipesa alikubali mashasrtoi hayo ya Bw. Kapongo na kumwacha mkewe na kurejea nyumbani.

Ilidaiwa kuwa siku ya pili mwanamke huyo alimweleza mumuwe kuwa usiku wakati amelala alishtukia mganga huyo ameingia katika chumba alimolala na kumbaka.

Hatua hiyo ilimfanya mwanamke huyo kupiga kelele lakini bila kupata msaada wowote.

Baada ya maelezo hayo, Bw. Kalipesa alimfuata mganga huyo na kumshushia kipigo kikali kilichosababisha kifo papo hapo.

Kwa mujibu wa Kamanda Mponguliana, watuhumiwa wote wa mauaji wanashikiliwa na Polisi mkoani hapa na watafikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa.

Wakati huo huo, mtoto Evance Sindani (8) mkazi wa Lunyara wilayani Nkasi, ameuawa kwa kugongwa na mkokoteni wakati akicheza barabarani.

Kamanda Mponguliana, alisema tukio hilo litokea Julai 19 saa 9 alasiri katika kijiji cha Lunyara.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.