Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Wafanyabiashara wa Soko Kkuu Kibondo wagoma kulipa kodi
Wafanyabiashara wa Soko Kkuu Kibondo wagoma kulipa kodi
By Prosper Kwigize | Published  07/26/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Mwandishi wa HabariTanzania.com, Kibondo

Wafanyabiashara wanaoendesha shughuli zao katika majengo ya soko kuu la mjini Kibondo mwishoni mwa wiki wametangaza kutolipa kodi mpya ya pango iliyotangazwa na halmashauri ya wilaya.

Maazimio hayo waliyatoa katika kikao cha pamoja cha wafanyabiashara na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo aliyewakilishwa na afisa biashara wa wilaya Bw. Sebastian Masuruli kilichofanyika mwishoni mwa wiki.

Wakitoa msimamo huo viongozi wa chemba ya biashara, kilimo na viwanda wilayani hapa TCCIA wamesema halmashauri ya wilaya imekuwa na desturi ya kujiamulia bila kuwahusisha walengwa wa huduma za jamii ambao ni wananchi.

Akiongea kwa niaba ya wenzao Bw. Plani Nzuguru amebainisha kuwa kodi imepanda kwa asilimia themanini hadi mia moja bila kuwahusisha watumiaji wa vyumba hivyo na kwamba halmashauri haijawalipa wafanyabiashara waliojenga baadhi ya vibanda katika soko hilo.

Bw. Nzuguru amebainisha kuwa vyumba vilivyokuwa vinalipiwa shilingi 4000 kodi imepanda hadi shilingi 8000 wakati vilivyokuwa vinalipiwa shilingi 8000 vimepandishwa hadi 15,000/=

Aidha wafanyabiashara hao wameleezea malalamiko yao kuwa waliojenga vibanda kuzunguka standi ya mabasi walikubaliana na halmashauri kutuma mthamini mjengo ili kuwekeana mikataba ya kupanga lakini tangu mwaka 1994.

Wameongeza kuwa halmashauri haijishughulishi hata kidogo kuvikarabati vibanda hivyo mbavyo baadhi vimechakaa licha ya kukusanya mapato kila mwezi kutoka kwa wapangaji wake.

Hata hivyo wafanyabiashara hao wamezirusha lawama zao kwa madiwani ambao ndio wanaodaiwa kupanga kiwango kipya cha kodi za halmashauri bila kuwahusisha wananchi wanaowawakirisha katika vikao vyao.

Awali akiongea kwa niaba ya mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya, afisa biashara wa wilaya Bw. Sebastian Masuruli amesema, wafanyabiashara wamekuwa na tabia ya kukwepa kodi ya pango na baadhi yao kuwabangisha wapangaji wapya bila kuzingatia taratibu.

Bw. Masuruli hakuwa tayari kuhojiwa na mwandishi wa habari ili kujua undani wa sakata hili na alimfukuza kwa kumtumia ujumbe nje kupitia kwa afisa mtendaji wa kata ya Kibondo Mjini kwa kile kinachoshiria ukiritimba na uongozi usiozingatia dhana ya utawla bora.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.