Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Wazazi Wilayani Kibondo washauriwa kupunguza kuzaa
Wazazi Wilayani Kibondo washauriwa kupunguza kuzaa
By Prosper Kwigize | Published  07/26/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Mwandishi wa HabariTanzania.com, Kibondo
Wazazi wameshauliwa kupunguza kasi ya kuzaa na badala yake wajiwekee mikakati endelevu ya kuwatunza watoto walionao ili kuondoa tatizo la watoto wa mitaani na ajira kwa watoto wao.
 
 Rai hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki na mwalimu wa taaluma wa shule ya sekondari ya wasichana Boni Consilii Mabamba Bw. Phares Peter wakati akihojiwa na mwandishi wa habari hii.
 
 Mwalimu Peter amesema tatizo la kuongezeka kwa watoto wa mitaani pamoja na watoto wanaoajiriwa ni matokeo ya wazazi kutopanga uzazi na kushindwa kabisa kuwalea watoto wao.
 
 Amebainisha kuwa baadhi ya watoto hushinikizwa na wazazi kuacha shule na kuingia katika ajira kama sehemu ya wazazi hao kukwepa majukumu ya malezi na baadhi yao huuchukua ujira wa watoto hao.
 
 Aidha kwa upande mwingine mwalimu wa taaluma wa shule hiyo amezitaka serikali za vijiji hadi ngazi ya wilaya kushirikiana na taasisi nyingine kutoa elimu kwa wazazi na kukomesha kabisa tatizo la wazazi kutelekeza watoto.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.