Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Dk. Nchimbi ahimiza habari zenye kujenga utamaduni
Dk. Nchimbi ahimiza habari zenye kujenga utamaduni
By Habari Tanzania | Published  05/18/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Na Eva Musiba, Mwanza
 
NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Emmanuel Nchimbi ametoa mwito kwa vyombo vya habari kuandika habari zenye kujenga utamaduni wa Mtanzania ili uheshimiwe na kulindwa kwa ajili ya vizazi vijavyo.
 
Aliyasema hayo juzi alipokuwa anatembelea vituo vya redio, televisheni na kampuni ya uchapaji magazeti ya CPPC ya jijini Mwanza.
 
Pia Naibu Waziri alikutana na waandishi wa habari wa mkoa wa Mwanza ambapo katibu wa chama cha waandishi wa habari mkoa, Jacob Kambili alisema kuwa kuna umuhimu wa serikali kuangalia uwezekano wa kurudisha utaratibu uliokuwepo wa maofisa habari wa mikoa.
 
Alisema malalamiko yanayotolewa na wadau mbalimbali wa habari juu ya baadhi ya waandishi, ambao ni wa kujitegemea, kutoaandika habari wakati wa ziara za viongozi yatamalizika tu pindi kutakapokuwa na maofisa hao, watakaokuwa waratibu wakuu.
 
Kambili alibainisha kuwa tatizo hilo linatokana na viongozi kumwita mwandishi mmoja mmoja, ambapo wakati mwingine sera ya gazeti inamhitaji kuandika habari sera inavyotaka na hivyo kulazimika baadhi ya habari kutoonekana.
 
Dk. Nchimbi aliwataka viongozi hao kuwa na ushirikiano na chama cha waandishi mkoa huu ili kupunguza malalamiko yanayojitokeza dhidi ya baadhi ya waandishi.
 
Naibu Waziri anaendelea na ziara katika mikoa ya kanda ya ziwa.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.