WANACHAMA watano wa chama cha Tanzania Labour Party (TLP), kinachoongozwa na Augustine Mrema, wamejiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kinachoongozwa na Freeman Mbowe.
Kaimu Katibu Mwenezi wa CHADEMA, Singo Benson aliwataja wapiganaji hao kuwa ni Walles Mkhoma, John Tendwa na Nicholas Mwakatobe.
Mwakatobe alikuwa mpishi wa Mrema tangu kiongozi huyo alipokuwa akiongoza chama cha NCCR-Mageuzi wakati Tendwa na Walles walikuwa walinzi wa kutumainiwa na Mrema, hasa kipindi cha kampeni za uchaguzi wa mwaka jana ambapo Mrema alikuwa mmoja wa wagombea wa urais.
Hata hivyo, Benson hakuwa tayari kutaja majina ya wanachama wengine wawili wa TLP waliohamia CHADEMA kwa madai kuwa wanaandaliwa hafla maalum ya kutangazwa rasmi.
Alisema wanachama hao wamehamia CHADEMA kwa madai kuwa chama chao (TLP), kinazidi kushuka umaarufu, hasa kutokana na migogoro ya mara kwa mara ndani ya chama hicho