Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mshirika wa Zombe mbaroni
Mshirika wa Zombe mbaroni
By Habari Tanzania | Published  07/26/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Na Asha Bani

MMOJA wa “vijana wa kazi” wanaotuhumiwa kushirikiana na aliyekuwa Kaimu Mkuu wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Abdallah Zombe, katika mauaji ya watu wanne, ametiwa mbaroni baada ya kujisalimisha.

Mtuhumiwa huyo, Koplo Festus Bwabisabi, sasa anaunganishwa na wenzake 11 kujibu mashitaka hayo ya mauaji ya wachimbaji madini watatu wa Mahenge mkoani Morogoro, na dereva teksi mkazi wa Dar es Salaam.

Baada ya kujisalimisha Kisutu, haraka haraka, polisi walimuunganisha katika kesi hiyo, na kumsomea mashitaka kama waliyosomewa wenzake.

Mbele ya Hakimu Mwandamizi Mfawidhi, Sivangilwa Mwangesi, Mwanasheria wa Serikali, William Magoma, alimsomea mtuhumiwa mashitaka manne yanayomkabili.

Magoma alidai kuwa, Koplo Bwabisabi anatuhumiwa kwa mauaji ya wafanyabiashara watatu wa wilayani Mahenge na dereva teksi wa kituo cha Sinza, Dar es Salaam; uhalifu ambao alidai kwamba watuhumiwa waliufanya Januari 14, 2005 maeneo ya Msitu wa Mbezi Louis, Dar es Salaam.

Magoma aliwataja waliouawa kuwa ni Ephaim Sabinus Chigambi, Sabinus Chigambi (Jongo), Mathias Lunkombe; na dereva wa teksi, Juma Ndugu.

Pamoja na Zombe ambaye ndiye mshitakiwa namba moja, wengine ni Christopher Bageni, Ahmed Makele, Noel Leonard, Jane Andrew na Koplo Nyangelela Morris.

Wengine ni Koplo Emmanuel Mabula; E.6712 Felix Sandys Cedrick; Koplo Michale; D.2300 Abeneth, PC Michael; Rashid Mahmoud Lema; na D/CPL Rajabu Hamis Bakari.

Watuhumiwa wote wapo katika mahabusu ya Ukonga. Kesho kesi yao itanguruma Kisutu.

Julai 13, mwaka huu, watuhumiwa 11, akiwamo Zombe walifikishwa Kisutu. Ilielezwa kwamba kesho watafikishwa mahakamani kwa ajili ya kusomewa maelezo ya mashahidi, tayari kwa kusikilizwa na Mahakama Kuu.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi, Sivangilwa Mwangesi, Mwendesha Mashitaka, Charles Kenyela, aliiambia mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika.

Alisema baadhi ya watuhumiwa walioomba kuandika maelezo ya nyongeza, wamekamilisha na maelezo hayo yameshawasilishwa kwa Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP), tayari kwa kusikilizwa katika Mahakama Kuu.

Waliokuwa wameomba kuandika maelezo ya ziada ni Ahmed Makele, Jane Andrew, Christopher Bageni, PC Konstebo Michael, D 2300 Abeneth na Noel Leornad.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.