Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mikopo ya wanafunzi yaichanganya serikali
Mikopo ya wanafunzi yaichanganya serikali
By Habari Tanzania | Published  07/25/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:
Na Deogratius Temba, SAUT

SERIKALI imesema itagharimia wanafunzi katika vyuo vya umma na binafsi waliofaulu vizuri.

Msimamo huo wa serikali ulitolewa jijini Dar es Salaam jana na Waziri wa Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Peter Msolla, alipozungumza na waandishi wa habari ili kutoa ufafanuzi wa utata ulioigubika jamii kwa siku kadhaa sasa.

Profesa Msolla, alisema kwamba wanafunzi waliofaulu vizuri, bila kujali wanasoma vyuo vya umma au binafsi, watagharimiwa mikopo.

Hata hivyo alitahadharisha kuwa wale wa vyuo vya binafsi watakaolipiwa ni wale waliofaulu vema, lakini wakakosa nafasi katika vyuo vya umma.

“Kwa kuwa serikali haina uwezo wa kusomesha kila mtoto kwa kiwango cha chuo kikuu, itatulazimu kutumia vizuri uwezo mdogo tulio nao.

“Kwa sasa msisitizo utakuwa ni kuwasomesha watoto waliofaulu vizuri zaidi, yaani wavulana katika kiwango cha daraja la I na wasichana katika kiwango cha daraja la I na II ili kuandaa wataalamu wengi zaidi kwa maendeleo ya taifa.

“Mikopo hii ni sawa na skolashipu ambazo duniani kote hutolewa kwa wanafunzi wanaofanya vizuri zaidi. Kwa hiyo utoaji wa mikopo utazingatia uwezo kitaaluma na uwezo wa kifedha wa serikali.

“Uwezo mdogo uliopo utumike kusomesha watoto katika kiwango cha juu  chuo kikuu kwa shahada ya kwanza tu (siyo shahada ya uzamili au falsafa).

“Ikitokea kwamba nafasi katika vyuo vikuu vya umma zimejaa, lakini bado kuna wanafunzi waliofaulu vizuri na wamekosa nafasi, serikali itawagharimia ipasavyo wanafunzi husika katika vyuo vikuu binafsi nchini.

“Hii ni njia mojawapo ya kupanua wigo wa udahili katika vyuo vikuu. Kwa kuwa taratibu za udhamini zimekiukwa na kusababisha wanafunzi wasiostahili kupata udhamini wa serikali, wanafunzi hao wataendelea na udhamini huo hadi wamalize masomo yao.

“Hata hivyo, kuanzia sasa, serikali itahakikisha kwamba wanafunzi watakaodhaminiwa na serikali ni wale tu wenye stahili hiyo kwa mujibu wa sheria,” alisema Profesa Msolla.

Alisema ili wanafunzi wengi waweze kufaidika na mikopo, serikali itaweka mipango ili wale walionufaika na mikopo hiyo, waanze kurudisha kuanzia mwaka huu wa fedha wa 2006/2007.

Kwa mujibu wa kanuni za mikopo, mwanafunzi anayestahili kupewa mkopo ni yatima, mlemavu au mwenye wazazi masikini na walemavu; anayetoka familia yenye mzazi mmoja masikini; anayetoka katika makundi yaliyotwezwa; na anayetoka familia yenye kipato duni.

Profesa Msolla alisema kuibuka kwa dhana kwamba mikopo ni ruzuku, matokeo yake ni shinikizo la kila mwanafunzi kutaka kukopeshwa asilimia mia moja hata katika maeneo ambayo walikuwa wanalipia wenyewe.

Matatizo mengine ni wanafunzi kujiandikisha zaidi ya chuo kimoja; na kubadili majina, akaunti, kuomba mkopo wakati ada imeshalipwa na wazazi au walezi, shirika na kadhalika


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.