Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mwenyekiti Arumeru arushiwa tuhuma
Mwenyekiti Arumeru arushiwa tuhuma
By Habari Tanzania | Published  07/24/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:
na David Frank

MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya Arumeru, John Saitabau, anatuhumiwa kuwakingia kifua ndugu zake wanaodaiwa kumjeruhi ndugu yao, Elias Saitabau, katika Kijiji cha Olgilai wilayani hapa.

Mwenyekiti huyo anadaiwa kuzuia mkono wa dola kuwakamata watuhumiwa hao licha ya tukio hilo kuripotiwa katika Kituo Kidogo cha Polisi Usa River na kufunguliwa jalada namba USR/IR/2378/06 Julai 12, mwaka huu.

“Angalia nilivyoumia kichwani, nimeshonwa nyuzi nane, kidoleni nyuzi mbili na tayari mgongo umetenguka hali inayonifanya nishindwe kuamka… yote haya yametokea baada ya mimi kuzuia miti yangu isikatwe,” alisema Elias ambaye yuko mafichoni akihofu kudhuriwa.

Aliongeza: “Nilipigwa mbele ya askari polisi watatu wa kituo kidogo cha Mbangata”.

Alidai kwamba waliompiga wote ni wanandugu, yaani Gabriel, Emmanuel na Hooshumu.

Akizungumza kwa njia ya simu na Tanzania Daima mwishoni mwa wiki, mwenyekiti huyo alikanusha tuhuma hizo.

“Siwakingii kifua kwa nia yoyote ile, na wala sihusiki kuwakamata na kuwafikisha mahakamani, suala hilo lipo polisi, naomba nisihusishwe kwa lolote,” alisema.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.