Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  CUF yakubali kuisamehe Marekani
CUF yakubali kuisamehe Marekani
By Habari Tanzania | Published  07/23/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Shabani Matutu

CHAMA cha Wananchi (CUF), kimekubali kuisamehe Serikali ya Marekani kwa kitendo cha kumshikilia mbunge wake wa Konde, Dk. Ali Tarab Ali katika Uwanja wa Ndege wa John F. Kennedy baada ya kumfananisha na gaidi anayesakwa na nchi hiyo.

Kaimu Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Mahusiano na Umma wa CUF, Mbaralah Maharagande, aliiambia Tanzania Daima jana kwa njia ya simu kuwa chama chake kimeipokea samahani iliyoombwa na Marekani.

Alisema wanasubiri kauli rasmi ya Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba ambayo itatolewa atakaporejea Dar es Salaam. Kwa sasa Profesa Lipumba yupo ziarani wilayani Lushoto.

“Tunasubiri tamko rasmi la mwenyekiti ambalo litatolewa kwa Watanzania wote atakaporejea kutoka Lushoto, tunatarajia kuandaa kikao maalumu cha chama ambacho kitatoa maamuzi ambayo yatakuwa rasmi,” alisema Maharagande.

Alisema kikao hicho pia kitapanga mikakati ya kuwalinda wabunge wake ili kuhakikisha kitendo hicho hakijirudii tena kwa viongozi wa chama hicho.

Maharagande alisema kitendo alichofanyiwa mbunge wake na maofisa usalama wa Marekani, hakikumuathiri yeye binafsi, bali kilikuwa na athari kubwa hata kwa chama chenyewe kwa kuharibu taswira yake.

Hivi karibuni, Balozi wa Marekani nchini, Michael Retzer alimwandikia barua ya kumuomba radhi, Spika wa Bunge, Samuel Sitta kutokana na kitendo kilichofanywa na maofisa usalama wa serikali ya nchi yake.

Katika barua hiyo, Retzer anaeleza kuwa, tukio hilo lilitokea kimakosa kutokana na kufanana kati ya Dk. Ali na gaidi anayesakwa na nchi hiyo.

Dk. Ali alikumbana na kashkash za Wamarekani alipokuwa amekwenda nchini Marekani, katikati ya mwezi Juni mwaka huu akiwa ameambatana na wabunge wengine watano katika msafara uliokuwa ukiongozwa na Waziri Mkuu, Edward Lowassa.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.