Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Kina cha maji Ruvu chapungua
Kina cha maji Ruvu chapungua
By Habari Tanzania | Published  07/23/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Na Martha Mtangoo, Dodoma

KINA cha maji katika Mto Ruvu kinaendelea kupungua kutokana na ukame, hivyo kuathiri uzalishaji wa maji katika mitambo ya Ruvu Juu na Ruvu Chini.

Akitoa taarifa katika semina ya wabunge kuhusu programu ya kitaifa ya maji na usafi wa mazingira vijijini mjini hapa jana kwa niaba ya Katibu Mkuu, Ofisa wa Wizara ya Maji, Mwinyikheri Ndimbo, alisema wizara inaendelea kutafuta vyanzo vipya, na kwamba matokeo ya utafiti wa awali unapendekeza ujenzi wa bwawa katika eneo la Kidunda mkoani Morogoro.

Kina hicho ndicho  chanzo kikuu cha maji kwa Jiji la Dar es Salaam na miji ya Kibaha na Bagamoyo.

Ndimbo alisema jumla ya sh bilioni 3.0 zitatumika kwa ajili ya kufanya utafiti wa kina na ujenzi wake unakadiriwa kugharimu jumla ya sh bilioni 70.

Kuhusu programu ndogo ya kuendeleza huduma za maji mjini, ofisa huyo alisema wizara yake inaendelea na uboreshaji wa huduma za maji katika Jijiji la Dar es Salaam na miji ya Kibaha na Bagamoyo ambao unatekelezwa kupitia mradi mkubwa wa ukarabati wa miundombinu ya maji safi na majitaka ambayo imechakaa na kupanua miundombinu kwenda kwenye maeneo ambayo hayajafikiwa na mtandao uliopo.  

Alisema mradi huo ulianza mwaka 2004 na unatarajiwa kukamilika mwaka 2008 kwa gharama ya jumla ya dola za Marekani 164.6 zitakazotolewa kwa pamoja na serikali, Benki ya Dunia, Benki ya Maendeleo ya Afrika na Benki ya Rasilimali ya Nchi za Jumuiya ya Ulaya.

Alisema kazi ya kukarabati mitambo ya Ruvu Juu na Ruvu Chini utekelezaji wake umefikia asilimia 40, ambapo kazi za ulazaji wa mabomba makuu mapya kutokana na vyanzo hivyo imefikia asilimia 30, lengo likiwa ni kulaza mabomba ya vipenyo kati ya milimita 150 na 600 yenye urefu wa kilometa 85,000 na kazi ya ulazaji wa bomba jipya linalomwaga majitaka baharini umefikia asilimia 94.

 Kuhusu programu ya kuendeleza huduma za Maji Vijijini, Ndimbo alisema utekelezaji wa programu ndogo ya maji vijijini katika miaka mitano ijayo utagharimu fedha kiasi cha sh bilioni 428.5.  

Alisema utekelezaji wa Sera ya Maji na mkakati wa kuendeleza huduma za maji vijijini utafanywa kupitia Programu ya Maji na usafi wa mazingira Vijijini utaotekelezwa kuanzia Julai mwaka huu, ambapo programu itatekelezwa kwenye ngazi ya wilaya kwa usimamizi wa Wizara ya Maji kwa kuzingatia misingi na mikakati ya sera ya taifa ya maji ya mwaka 2002.

 Awali akifungua semina hiyo, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Samuel Sitta, alisema programu hiyo ya kuendeleza maji vijijini itafanikisha upatikanaji wa huduma endelevu ya maji vijijini.

Alisema tofauti na hapo zamani ambapo wataalamu walikuwa wakiandaa mipango na kujenga miradi na kuiendesha pasipo kushirikisha wanachi, utaratibu ambao kwa kiasi kikubwa umechangia katika kuchelewesha upatikanaji wa huduma endelevu ya maji vijijini.

Spika alisema programu hiyo imezingatia ushirikishwaji wa wananchi ambao ndio watakaoibua miradi, kuipanga, kuitekeleza na kuiendesha.

 Naye Waziri wa Maji, Stephen Wassira, alisema lengo la programu hiyo ni kutoa huduma ya maji kwa asilimia 100 kwa wakazi wote wa vijijini ifikapo mwaka 2025


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.