Habari Tanzania - http://www.habaritanzania.com
Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
http://www.habaritanzania.com/articles/6/1/Ghorofa-Jijini-lanusurika-kuungua-moto
By Habari Tanzania
Published on 05/9/2006
 

Nyumba ya ghorofa moja iliyopo Karikoo Jijini katikati ya mitaa ya Kongo, Ndovu na Rufiji nusura liungue kwa moto.


Nyumba ya ghorofa moja iliyopo Karikoo Jijini katikati ya mitaa ya Kongo, Ndovu na Rufiji nusura liungue kwa moto.

Watu walioshuhudia moto huo wamesema chokochoko zilianzia kwenye ghorofa ya chini ya jengo hilo.

Wamesema chanzo cha moto huo ambao ulizimwa na Kikosi cha Kuzima Moto cha Jiji kabla haujaleta madhara ni hitilafu ya umeme.

Wakazi wa maeneo jirani na nyumba hiyo wamesema kama moto huo usingedhibitiwa mapema, ungeweza kuleta kasheshe kubwa kutokana na eneo hilo kuwa na majengo mengi na kuwa lenye heka heka nyingi za biashara.

Sababu nyingine iliyowafanya watu hao kuwa na hofu kubwa ni jirani na jengo hilo kuwa na ghala la kuuzia mkaa.

’Ni hatari sana kuuza mkaa karibu na makazi ya watu, kama moto usingedhibitiwa mapema ungeweza kuleta madhara makubwa,’ mmoja wa watu walioshuhudia amesema.

Habari zaidi kutoka kwenye tukio zinasema moto huo umesababisha uharibifu wa vifaa mbalimbali vilivyoko ndani ya jengo hilo ikiwa ni pamoja na kiyoyozi.
  • SOURCE: Alasiri