Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Majambazi wapora watalii K’njaro
Majambazi wapora watalii K’njaro
By Habari Tanzania | Published  07/21/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Na Charles Jacob, Moshi

WATU wanaodhaniwa kuwa majambazi, wamevamia basi lililosheheni watalii wilayani Siha na kuwapora mali na fedha taslimu.

Tukio hilo lilitokea jana mchana wakati watalii hao wakienda kutoa msaada katika Kanisa la International Evangelical lililopo Engale Nairobi wilayani Siha.

Watuhumiwa hao wa ujambazi walitumia pikipiki katika uporaji huo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Hai, Daniel Sandewa, alizungumza na Tanzania Daima kwa simu na kuthibitisha kuwapo kwa tukio hilo.

Alisema RCO wa Mkoa wa Kilimanjaro, Hezron Kigonda, hadi jana jioni, alikuwa eneo la tukio, akiongoza operesheni ya kuwasaka watuhumiwa hao.

Alisema pamoja na pesa, vitu vingine vilivyoporwa ni kamera, simu selula na zawadi mbalimbali zilizokuwa zikipelekwa katika kanisa hilo.

Habari zilizopatikana baadaye zilisema baada ya uporaji huo, watuhumiwa walijificha katika msitu wa West Kilimanjaro.

Polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), walipelekwa eneo hilo kwa kazi moja ya kuwasaka na kuwanasa majambazi hao.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.