Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Aliyepigwa na Wapakistani azidiwa Muhimbili
Aliyepigwa na Wapakistani azidiwa Muhimbili
By Habari Tanzania | Published  07/20/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Asha Bani

HALI ya mgonjwa aliyepigwa na wawekezaji Wapakistani katika Kiwanda cha Nguo cha NIDA, cha Dar es Salaam ni mbaya.

Mgonjwa huyo, Adinani Khalifa (26), ambaye amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN), wodi ya Mwaisela, anasumbuliwa na tatizo la kutokwa mkojo mfululizo pamoja na maumivu ya nyonga ya mguu wa kushoto.

Hali ya mgonjwa huyo ilidhihirika kuwa ni mbaya jana baada ya Hakimu Mkazi wa Kisutu, Eddy Lyamuya, akiongozana na Mwendesha Mashitaka, Charles Kenyela, kwenda kumwona Muhimbili ili atoe uamuzi wa kuwapa au kuwanyima dhamana watuhumiwa hao, raia wa Pakistan.

Mbali ya kutembelea Hospitali ya Muhimbili kuona hali ya majeruhi aliyepigwa, mahakama hiyo pia ilikwenda katika Zahanati ya  Apollo Medical Center iliyopo Mtaa wa Mshihiri, Barabara ya Morogoro  kumsomea mashitaka mtuhumiwa, Inamu Shamrey Khani (25), ambaye anasumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu kutokana na mshituko wa kutiwa mbaroni kwa tuhuma za kumpiga Khalifa.

Khani  ni mkuu wa umaliziaji katika uzalishaji kiwandani hapo na amelazwa tangu juzi, na jana alisomewa mashitaka mawili, la kwanza la kumpiga kwa kutumia kipande cha chuma na kumsababishia maumivu Khalifa, na shitaka la pili ni la kumvunja nyonga na kumsababishia maumivu ya jicho la upande wa kushoto na kumfungia ndani ya kontena.

Katika kesi hiyo watuhumiwa wanadai  hawajui lugha yoyote ila Kipakistani, hivyo wanatumia mkalimani kupata mawasiliano mahakamani.

Lakini baada ya mahojiano na mgonjwa Adinani, ilidaiwa kuwa, watuhumiwa wanajua lugha nyingine ikiwa ni pamoja na Kiswahili, Kiingereza na Kipakistani, hata wakati wakimpiga walikuwa wana mtukana matusi kwa lugha ya Kiswahili.

Katika kesi hiyo iliyoanza kusikilizwa juzi, watuhumiwa ni Habibu Khani (30), afisa masoko, Mohamed Rashid (25), mtunza stooo, Shazad Hassani Khani (36), Inamu Shamrey Khani (25), mkuu wa kitengo cha uzalishaji na Mohamed Khalifa (30), mwendesha mitambo.

Watuhumiwa hao wanaongozwa na wakili Justinian Lyabato, ambaye aliwaombea dhamana lakini mahakama ilikataa ombi hilo kutokana na hali ya mgonjwa  kuwa mbaya.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.