Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Wakurugenzi nchini kote wapanguliwa
Wakurugenzi nchini kote wapanguliwa
By Habari Tanzania | Published  07/20/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:
Na Tamali Vullu, Dodoma

SERIKALI imepanga upya safu ya wakurugenzi wa halmashauri kwa kufanya uteuzi wa wakurugenzi wapya 37 watakaoziba nafasi zilizo wazi na kuwaondoa kwenye wadhifa huo wakurugenzi 25.

 Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mizengo Pinda, alisema wakurugenzi 32 wamehamishwa kwenda vituo vipya na wakurugenzi 53 wataendelea kufanya kazi katika vituo vyao vya zamani.  

“Serikali inaagiza wakuu wa mikoa yote inayohusika kusimamia vema makabidhiano, ili lifanyike ipasavyo na kwa ufanisi kwa kuzingatia taratibu husika,” alisema.  

Wakurugenzi wapya na halmashauri zao zikiwa kwenye mabano ni Dk. Job Laiser (Arusha), Shaban Ntarambe (Kigoma Ujiji), Sendui ole Nguyaine (Sumbawanga), Hassan Mwanziku (Tabora), Kimulika Galikunga (Lindi) na Ahamed Sawa (Korogwe).

Wakurugenzi wa halmashauri za wilaya ni Glady Dyamvunye (Mpwapwa), Mary Qorro (Kondoa), Jackson Samwel (Kongwa), Bosco Nduguru (Kilolo), Tina Senkambo (Iringa), Consolata Kamuhabwa (Karagwe), Ernest Bagaya (Muleba), na Ally Kombo (Bukoba).

Wengine ni Samwel Sarianga (Kigoma), Francis Namaumbo (Kasulu), Paulo Nkulila (Kibondo), Esau Sigalla (Same), Nichalaus Mtega (Hai), George Moya (Liwale), Athuman Akalama (Ruangwa), Jude Mboya (Kilwa), Hijob Shenkalwa (Lindi),  Juma Idd (Bunda) na Karaine Kunei (Musoma).

Wengine ni Henry Haule (Simanjiro), Naijajaya Koira (Mbulu), Alfred Luanda (Ulanga), Leonard Masale (Ukerewe), Hassan Mwachibuzi (Mkuranga), Azimina Mbilinyi (Rufiji), Deogratias Hela (Kibaha), Illiminata Mwenda (Tunduru),  Mruma Athman (Songea), Sylivia Siriwa (Nzega), Neneka Rashid (Pangani), na Lilian Matinga (Korogwe).

Wakurugenzi wa halmashauri za manispaa walioondolewa kwenye nafasi hizo na kupangiwa kazi nyingine ni Noah Mwaikuka aliyekuwa Arusha; Monica Kwiluhya (Dodoma), Laban Tanda (Kigoma/Ujiji), Desderius Narwango (Sumbawanga) na Fedilia Khalfan (Tabora).  

Kwa mujibu wa Pinda, wakurugenzi wa halmashauri za miji walioondolewa ni Malima Muya (Lindi) na kwa upande wa wakurugenzi wa halmashauri za wilaya walioondolewa ni Freddy Masele (Kondoa), Gideon Manambo (Mpwapwa), Mabala Mboje (Karagwe), Mohamed Masha (Kigoma), Brown Kintungi (Liwale), Thabitha Mshakangoto (Kilwa) na Cyprian Mwita (Lindi).  

Wengine walioondolewa ni Januarius Gasembe (Simanjiro), Wilhelm Tsere (Mbulu), Yohana Tessua (Musoma), Method Marwa (Ulanga), Henry Uisso (Mtwara), Anthony Mageka (Ukerewe), Serena Chidumizi (Rufiji), David Kilonzo (Mkuranga), Metern Shirima (Kibaha), Joyce Mbutta (Maswa), Samuel Mashindike (Igunga), na Verdiana Mushi (Sikonge).  

Wakurugenzi wa halmashauri za jiji waliobadilishwa vituo vya kazi na vituo vyao vipya vikiwa kwenye mabano ni Elizabeth Munuo aliyekuwa Tanga (Mbeya); Wilson Kabwe-Mbeya (Mwanza), na Paulo Baruti-Mwanza (Tanga).

Wakurugenzi wa halmashauri za manispaa waliohamishwa na vituo vyao vipya vikiwa kwenye mabano ni Susan Bidya-Halmashauri ya Wilaya Dodoma (Dodoma), Bernadetha Kinabo-Halmashauri ya Manispaa Singida (Singida), na Robert Kitiombo-Halmashauri ya Wilaya Moshi (Singida).

 Kwa mujibu wa Pinda, wakurugenzi wa halmashauri ya wilaya waliohamishwa na vituo vyao vipya vikiwa kwenye mabano ni Cprian Oyier-Muleba (Karatu), Zuberi

Mbyana-Bukoba (Ngorongoro), Jane Senga-Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni (Dodoma), Hadrian Kayombo-Kasulu (Makete), Castory Tingirawanyuma-Songea (Ngara), Ester Mbigili-Korogwe (Moshi), Theresia Mmando-Kilosa (Rombo), Maiko Seepunjo-Korogwe (Mwanga).

   Wengine ni Nachoa Zacharia-Ruangwa (Serengeti), Levisson Chilewa-Mwanga (Mbozi), Maurice Sapanjo-Morogoro (Chunya), Anna Mwahlende-Chunya (Morogoro), Ahmed Mshamu-Tunduru (Kilosa), Jarvis Simbeye-Geita (Mtwara), Dani Mollel-Shinyanga (Geita), Amir Gwakiray-Maria (Kisarawe), Lewis Kalinjuna-Kisarawe (Mafia), Majuto

Mbuguyu-Mbozi (Mbinga), Pius Affa-Urambo (Shinyanga), Gabriel Fuime-Iringa (Maswa), Agness Kitundu-Nzega (Manyoni), Anunciata Lyimo-Kilindo (Singida), Nicholaus Kilela-Ngorongoro (Igunga), Jim Mlay-Kongwa (Sikonge), Justus Molai-Bunda (Urambo) na Kilonzo Bwelela-Serengeti (Kilindi).  

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Bakari Kingobi, amebakizwa kwenye kituo chake cha zamani.

Wakurugenzi wa halmashauri za manispaa waliobaki kwenye vituo vyao ni Iddi Nyundo (Temeke), Hussein Katanga (Kinondoni), John Lubuva (Ilala), Abubakar Midelo (Iringa), Faustine Fissoo (Bukoba), Theones Nyamahanga (Musoma), Raphael Ndunguru

(Morogoro), Fredrick Ntakabunyula (Mtwara), Edgar Berege (Songea) na Folkward Kapinga (Shinyanga).

Wakurugenzi wa halmashauri za miji waliobaki ni Lameck Masembejo (Babati) na Tabu Ernest (Kibaha).

Wakurugenzi wa halmashauri za wilaya waliobaki vituo vya zamani ni Eden Munisi (Monduli), Raphael Mbunda (Arumeru), Mohamed Mkupete (Njombe DC), Sabin Sirima (Ludewa DC), Halfa Hida (Mufindi (DC), William Mgalula (Biharamulo DC), Tresius Kagenzi (Nachingwea DC), Andrew Juma (Kiteto DC), Philbert Ngaponda (Babati DC),

Limbakisye Shimwela (Hanang), George Kagomba (Tarime DC), Mashanga Bulilga (Rungwe DC),  Shaibu Muyinga (Mbarali DC), Sarah Linuma (Kyela DC), Yona Maki (Ileje DC), Mhando Senyagwa (Mvomero), Theresia Mahongo (Kilombero), Noah Mahyenga (Masasi

DC), Alquin Ndungwi (Newala DC), Gebra Msuya (Tandahimba), Sebastian Masso (Sengerema), Lucas Buremo (Magu), Jeane Mutagurwa (Kwimba) na Rose Elipenda (Misungwi).

Wengine ni Rhoda Nsemwa (Bagamoyo), Mussa Zungiza (Sumbawanga DC), Denis Bandisa (Mpanda DC), Dk. Vallery Kessy (Nkasi DC), Willy Njau (Namtumbo DC), Paul Kihwele (Meatu DC), Theonest Kishenyi (Bukombe DC), Christine Midello (Kishapu DC), Goody Pamba (Kahama DC), Kyuza Kitundu (Bariadi), Dk. Izidor Mtalo (Iramba DC), Dorothy

Rwiza (Uyui DC), Ephrem Kalimalwendo (Muheza DC), Obedi Mwasha (Lushoto DC) na Mpangalukela Tatala (Handeni DC).


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.