Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Lowassa: Sasa kazi iwe kukuza kilimo, semina za maboresho ya halmashauri zisimamishwe
Lowassa: Sasa kazi iwe kukuza kilimo, semina za maboresho ya halmashauri zisimamishwe
By Habari Tanzania | Published  05/19/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Na Mwandishi Wetu
 
WAZIRI Mkuu, Edward Lowassa, amewaagiza viongozi wa halmashauri za miji nchini kusimamisha semina za maboresho, na nguvu zote zielekezwe katika kuinua kilimo ndani ya maeneo yao.
 
Lowassa alitamka hayo jana katika majumuisho ya mkutano wa wadau wa kahawa nchini uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam, ambao pia ulikuwa ni hitimisho la mikutano ya wadau wa mazao ya kilimo iliyofanyika kwa wiki moja.
 
Mikutano mingine ilihusisha mazao ya korosho (Ijumaa), pamba (Jumatatu) na juzi ulikuwa wa tumbaku.
 
“Wakurugenzi (wa halmashauri), madiwani na maofisa wa watendaji wa kata, nasema semina za maboresho sasa basi, sana sana pawepo na ulazima mkubwa,” alisema Lowassa na kuongeza:
 
“Wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa, sasa fanikisheni kilimo kama mlivyofanikisha ujenzi wa madarasa ya sekondari. Sitaki visingizio, katibu kata kafanya hivi na vile, wote hawa wako chini yenu. Tuanzie hapo, atakayeshindwa tutajua mbele ya safari tutafanya nini.”
 
Katika mkutano huo, Lowassa aliagiza ifanyike mikakati ya kuongeza uzalishaji wa kahawa nchini kufikia tani 120, 000 ifikapo mwaka 2010, kutoka tani 54,000 za sasa kwa mwaka. Malengo ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika yaliyosomwa awali na Waziri wa Kilimo na Chakula, Joseph Mungai, ni kuzalisha tani 100,000 katika kipindi hicho.
 
Kuhusu suala la soko, Waziri Mkuu aliagiza wananchi wahamasishwe kuwa na tabia ya kunywa kahawa, baada ya Mungai kusema kuwa soko lake nchini ni dogo mno.
 
Mungai alisema kuwa serikali imewekeza kiwango kikubwa cha pesa katika kilimo cha kahawa, jambo ambalo litasaidia kupunguza makali ya gharama za uzalishaji kwa mkulima na kumpatia faida kubwa.
 
Pia waziri huyo alizitaka halmashauri kupunguza kodi za mazao, jambo ambalo nalo litampa unafuu katika uzalishaji wake.
 
Waziri Mkuu aliitaka wizara inayohusika na kilimo na wadau wengine kuangalia namna ya kusimamia bei ya zao hilo, ili kufikia lengo la kahawa anayoizalisha mkulima ifikie walau asilimia 70 ya soko la dunia.
 
Akichangia mada, Waziri wa Miundombinu na mbunge wa Rombo, Basil Mramba, aliyejitambulisha kama mkulima mdogo, alisema kuwa tatizo la uzalishaji mdogo wa kahawa ni kutokana na mibuni iliyozeeka ambayo inazalisha asilimia 20 ya uwezo halisi.
 
Mramba alisema uamuzi mgumu wanaoupata wazalishaji wa kahawa ni iwapo watang’oa mibuni na ndani ya miaka mitano wakati inakua, watakula nini.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.