Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Hali ya Hewa watakiwa kubadilika, kwenda na mabadiliko ya teknolojia
Hali ya Hewa watakiwa kubadilika, kwenda na mabadiliko ya teknolojia
By Habari Tanzania | Published  07/19/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Na Mwandishi Wetu
 
WAZIRI wa Miundombinu Basil Mramba, ameitaka Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) kubadilisha utendaji kazi na kuanza kutoa taarifa za hali ya hewa katika muda wa kuanzia dakika moja, saa, siku, wiki hata mwaka ili kwenda na teknolojia inayobadilika duniani.
 
Mramba alisema hayo juzi alipokuwa akifungua warsha ya kimataifa ya watalaamu wa hali ya hewa kutoka Afrika, India, Marekani na Ulaya iliyofanyika jijini Dar es salaam.
 
Warsha hiyo imeandaliwa na TMA na kufadhiliwa na Mradi wa Hali ya Hewa Duniani (CLIVAR) wakishirikiana na Shirika la Hali ya Hewa Ulimwenguni (WMO).
 
Mramba alisema TMA kwa sasa inao watalaamu wa kutosha, lakini tatizo ni vifaa vya kisasa vinavyoweza kugundua mabadiliko ya hali ya hewa au kubashiri tukio au janga la miaka mitano ijayo.
 
"Serikali ya awamu ya nne imeliona tatizo hilo na tayari imetenga sh. bilioni 1.7 ili kununua 'radar' ya kuangalia hali ya hewa," alisema na kuongeza kwamba fedha hizo zilipitishwa na wabunge walipojadili makisio ya wizara yake.
 
Alisema kifaa hicho kitasaidia kuona mabadiliko ya hali ya hewa kwa muda wowote katika eneo litakalofikiwa.
 
Kufuatia uamuzi hu, Waziri Mramba aliwataka wafanyakazi wa TMA kujiweka tayari kubadilika kwa kutoa taarifa mapema na kuzisambaza kwa kasi.
 
Akizungumzia hali ya hewa kwa ujumla, Mramba alisema masuala hayo yanahitaji ushirikiano wa karibu na nchi mbalimbali duniani ili kugundua mabadiliko yanapotokea.
 
Alisema Tanzania tayari ilishapata maafa ya hali ya hewa kwa kukumbwa na El nino, lanino, ukame na hata kuchelewa kwa mvua jambo ambalo kwa kawaida lilitakiwa kutolewa tahadhari mapema.
 
Mkurugenzi wa TMA Dk. Mohammed Mhita akizungumza kwenye hafla hiyo, aliishukuru serikali kwa kutenga fedha za kununua radar ambayo alisema itakuwa ya kwanza ya aina yake tangu nchi ipate Uhuru.
 
Alipoulizwa ni lini radar itanunuliwa, Dk. Mhita alisita kuutaja kwa maelezo kwamba ofisi yake itatakiwa kukaa na kuandaa utaratibu wa ununuzi wake.
 
Alisema kabla ya Uhuru Tanzania ilikuwa na radar nne zilizokuwa Mwanza, Mtwara, Dare s Salaam na Iringa lakini radar zote ziliharibika na kusababisha matukio mengi ya mabadiliko ya hewa kupita bila kutabiriwa.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.