Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Waacha kujenga kituo cha polisi wakihofia watoto wao kufungwa
Waacha kujenga kituo cha polisi wakihofia watoto wao kufungwa
By Habari Tanzania | Published  07/19/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Na Selina Wilson, Kibaha
 
WANANCHI wameacha kuchangia ujenzi wa kituo cha polisi kwa kuhofia watoto wao watawekwa ndani kitakapokamilika.
 
Ujenzi wa Kituo cha Polisi cha Mwendapole kata ya Kibaha mkoani Pwani umekwama kwa miaka miwili sasa.
 
Hofu hiyo inatokana na baadhi ya vijana katika eneo hilo kujihusisha na matukio ya uhalifu na kwamba wazazi wao wamekuwa wakiwategemea kuwapatia riziki kutoka na kazi hiyo isiyo halali.
 
Mwenyekiti wa mtaa wa Mwendapole Mbarouk King`wenyu alisema hayo wakati akizungumza na mwandishi wa habari hii kuhusu maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho ambacho ulianza mwaka 2002, na kutarajiwa kukamilika 2004.
 
Alisema uamuzi wa kujenga kituo hicho ulifanywa na wananchi wenyewe baada ya kukithiri kwa vitendo na matukio ya uhalifu yanayotokea kijijini hapo, hivyo waliona njia pekee ni kuwepo na kituo cha polisi.
 
King`wenyu alisema matukio mengi ya wizi na uporaji mdogo mdogo yanasababishwa hasa na vijana ambao ni wakazi wa kijiji hicho na baadhi yao hupata upenyo wa kufanya uhalifu kutokana na kukosekana kwa polisi karibu na kijiji hicho.
 
Alisema baada ya kupitisha uamuzi huo, walikubaliana kila kaya ichangie sh. 300 huku serikali ya mtaa ikiendelea kutafuta wafadhili wa kusaidia ujenzi huo, lakini baadaye mambo yalikuwa kinyume na kaya zilikwama kuchangia na hivyo kuzorotesha ujenzi huo mpaka sasa.
 
Mwenyekiti alisema hali ya usalama katika mtaa huo haikuwa nzuri, lakini bado wazazi walikuwa wazito kuchangia nguvu zao kujenga kituo na hata sasa tatizo kubwa linasumbua mtaa huo ni uhalifu unaofanywa na vijana wa eneo hilo.
 
Alisema mpaka sasa kuna baadhi ya vijana wamefungwa jela na wengine bado wanatafutwa huku serikali ya mtaa ikiendelea kudhibiti matukio ya uhalifu kwa kushirikiana na polisi.
 
Akizungumzia ujenzi wa kituo hicho, alisema umefikia katika hatua ya madirisha na bado kufikia linta na mpaka hapo umegharimu zaidi sh. 500,000 hivyo wameomba wafadhili wajitokeze kusaidia.
 
Pia, ametoa wito kwa wananchi wa eneo hilo kubadili mawazo ili waendeleze ujenzi huo.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.