Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  MIKATABA YA MADINI:Wabunge wataka tume iundwe upesi
MIKATABA YA MADINI:Wabunge wataka tume iundwe upesi
By Habari Tanzania | Published  07/19/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
 Wasema ndiyo itakayofumbua ukweli wa mambo
 
Wanasheria walaumiwa kuwa chanzo cha utata
 
 Selelii aibuka tena na kuonya unyanyasaji migodini
 
Na Dunstan Bahai, Dodoma
 
WABUNGE wameshauri iundwe Tume ya kuchunguza mikataba mbalimbali ya madini na wanasheria wamelaumiwa kuwa chanzo cha mikataba yenye utata.
 
Ushauri huo ulitolewa jana na baadhi ya wabunge waliochangia mjadala wa hotuba ya makadirio na matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini iliyowasilishwa na waziri wake, Dk. Ibrahim Msabaha. Katika ushauri wao wametaka Tume iwajumuishe wabunge.
 
Mbunge wa Nzega (CCM) Lukas Selalii alisema kuundwa kwa tume hiyo ndiyo kutakakoeleza ukweli wa matatizo yaliyopo kwenye mikataba ya madini.
 
Alisema mikataba mingi imekuwa ikiwanufaisha zaidi wawekezaji ambapo utakuta eneo lina utajiri mkubwa wa madini, lakini wananchi wake ni masikini wa kutupwa.
 
Selalii alilalamikia kitendo cha wafanyakazi wazawa katika migodi ya madini kunyanyaswa na wawekezaji ikiwa ni pamoja na kulipwa mishahara midogo ikilinganishwa na wawekezaji wenyewe hata kama wana sifa zinazolingana.
 
Ili kunusuru madini yanayoporwa na wageni, mbunge huyo alishauri kwamba TRA wangekuwa wasimamizi wakubwa wakati wa kuchimba hadi hatua ya mauzo.
 
Hata hivyo, alilaumu kwa muda mrefu wanasheria kuwa ndiyo chanzo cha kuwa na mikataba yenye utata.
 
Aliiomba serikali kuwa kama kuna uwezekano tume hiyo ikiundwa na ikibainika wanasheria ndiyo chanzo, basi nao wachukuliwe hatua kali za kisheria.
 
Dk. Wilbrod Slaa (Karatu-CHADEMA) aliomba kuharakishwa kuundwa kwa tume hiyo na Taasisi ya Kuzuia Rushwa (PCB) nayo iingilie kati kwenye mikataba hiyo.
 
Hata hivyo, aliiomba wizara kuboresha huduma ya umeme ambapo pia alishangazwa pamoja na mvua kunyesha katika maeneo ya mabwawa kama la Mtera, lakini kuna mgao wa umeme.
 
Alisema kama tatizo ni la wataalamu walioliachia bwawa hilo kujaa mchanga, basi wachukuliwe hatua kali.
 
Lucy Owenya (Viti Maalum-Chadema) naye alihoji ni kwa nini kuna mgawo wa umeme huku mabwawa hayo yakiwa yamesheheni maji.
 
Beatrice Shellukindo (Kilindi-CCM) alisema Tanzania ni tajiri, lakini wananchi wake ni masikini wa kutupwa.
 
Hata hivyo, aliipongeza wizara kwa kazi nzuri lakini alisema baadhi ya watendaji wanazorotesha jitihada za wananchi za kujiondolea umasikini na kuwakumbatia wawekezaji wageni.
 
Mbunge wa Njombe Kaskazini (CCM) Jackson Makwetta aliipongeza Tanesco kwa kazi nzuri na kuwataka wanaolaumu utendaji huo wakumbuke pia kuwa kama mashirika mengine na lenyewe linafanya kazi nzuri pamoja na kwamba ni katika mazingira magumu.
 
Aliiomba serikali kuliwezesha shirika hilo ili limudu majukumu yake na kwamba endapo litaachwa na kufa, hakutakuwa na shirika lingine mbadala
 
 

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.