Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Lupogo ahimiza vita ya Ukimwi makazini
Lupogo ahimiza vita ya Ukimwi makazini
By Habari Tanzania | Published  07/17/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Meja Jenerali (Mstaafu) Herman Lupogo, ameiasa jamii ya wafanyabiashara nchini kuwa na sera nzuri za mapambanano dhidi ya Ukimwi makazini ili kulinda nguvu kazi dhidi ya ugonjwa huo.

Meja Jenerali Lupogo aliyasema hayo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam kwenye kilele za matembezi ya hisani ya wafanyakazi wa Kampuni ya Sigara Nchini (TCC).

Matembezi hayo yaliandaliwa ili kuchangia fedha kwa ajili ya vita dhidi ya Ukimwi kwa jamaa za wafanyakazi kampuni hiyo.

Alisema ikiwa kampuni yoyote inafanya biashara kwenye jamii iliyozungukwa na ugonjwa huu wa Ukimwi, basi biashara ya pili ya kampuni hiyo ni kupambana na ugonjwa huo ili usijekuiharibu biashara ya kwanza.

’’Nimefurahishwa sana na sera yenu dhidi ya Ukimwi, iko wazi ikilenga kuwakinga wafanyakazi wenu dhidi ya ugonjwa huu?cha muhimu hapa ni kuhakikisha mnayatekeleza haya malengo mazuri yaliyomo humu,’’ alisama Bw. Lupogo.

Bw. Lupogo ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye matembezi hayo ya kilomita tatu, yakianzia makao makuu ya TCC mpaka kwenye klabu ya TCC Chang’ombe alisema ni jambo zuri kwamba wafanyakazi wameamua kuzikumbuka familia zao kwenye elimu dhidi ya Ukimwi kwani ugonjwa huo ni wa jamii nzima.

Alisema ajuavyo yeye ni kwamba yako makampuni mengi yenye kufundisha wafanyakazi wao elimu ya Ukimwi, bado hajaona makampuni yenye kuziingiza familia kwenye elimu ya ugonjwa huo kama walivyofanya TCC.

Kwa upande wake, Bw Da Motta aliishukuru serikali kwa kutambua juhudi za makampuni binafsi za kupambana na Ukimwi.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.