Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mwenyekiti NLD aipa changamoto serikali
Mwenyekiti NLD aipa changamoto serikali
By Habari Tanzania | Published  07/16/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Agnes Yamo

MWENYEKITI wa taifa wa Chama cha NLD, Dk. Emmanuel Makaidi, amesema kupanda kwa mishahara hakutakuwa na maana kama serikali itashindwa kudhibiti upandaji wa gharama za maisha.

Mwenyekiti huyo alitoa maoni hayo jana alipofanya mahojiano maalumu  na  Tanzania Daima, Dar es Salaam.

“Bajeti hii haimsaidii mwananchi wa kawaida, kwani kupata hiyo shilingi laki moja kisha ukapandisha gharama za umeme, chakula, maji, fedha hiyo haitamudu gharama hizo,” alisema

Alisema bajeti inatakiwa iwe na malengo maalumu kwa kubadilisha maisha kwa watu wenye kipato cha chini kuweza kumudu gharama za msingi na kujiwekea akiba kwa maisha ya baadaye

Aliishauri serikali kutumia mawazo ya wapinzani wenye nia moja ya kuhakikisha kuwa nchi inasonga mbele kimaendeleo.

“Si busara kulaumu serikali kila wakati, tuko tayari kushirikiana na serikali iliyoko madarakani, ikiwa ni pamoja na kushauri pale wanapokwenda,” alisema.

Akizungumzia suala la ruzuku ya sh milioni 500 iliyotolewa kwa kila mkoa kwa lengo la kuondoa umaskini, Dk. Makaidi alisema haitawasaidia kwani ni kiasi kidogo.

“Hizo milioni 500 kwa kila mkoa ni  kiini macho, haiwezekani kuondoa umaskini kwa milioni 500 kwa kila mkoa, mtawakopesha watu wangapi?” alihoji Dk. Makaidi.

Alishauri serikali kutenga sh bilioni tano kwa kila mkoa badala ya sh milioni 500 ambazo zitaleta urasimu wakati wa kukopesha.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.