Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Wajue viongozi wapya wa TEC
Wajue viongozi wapya wa TEC
By Habari Tanzania | Published  07/16/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Mwandishi Wetu

BARAZA la Maaskofu Tanzania (TEC) sasa lina sura mpya. Lilipata viongozi wapya, akiwamo Rais wake, Askofu Yuda Thadei Ruwa’Ichi wa Jimbo la Dodoma.

Ruwa’Ichi anachukua nafasi ya Askofu Severin Niwemugizi wa Rulenge anayeondoka kutokana na kumaliza muda wake. Askofu Mkuu Norbert Mtega wa Songea, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Idara ya Elimu alichaguliwa kuwa Makamu wa Rais.

Katika uongozi huo mpya, yupo Padri Anthony Makunde, anayekuwa Katibu Mtendaji, akichukua nafasi ya Padri Dk. Pius Rutechura, ambaye kwa sasa ana wadhifa wa Katibu Mtendaji wa AMECEA, mwenye ofisi yake jijini Nairobi, Kenya.

Wote hao na wengine ambao ni wenyeviti wa idara mbalimbali, walichaguliwa katika mkutano wa 59 wa TEC. Wenyeviti hao ni Askofu Msaidizi, Dk. Method Kilaini (Fedha na Mipango), Askofu Amedeus Msarakie wa Moshi (Uchungaji), Askofu Jacob Koda wa Same (Utume ), Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa wa Iringa (Liturjia) na Askofu Agapit Ndorobo wa Mahenge (Caritas).

Wengine ni Askofu Aloysius Balina wa Shinyanga (Afya), Askofu Telesphor Mkude wa Morogoro (Katekisi) na Askofu Alfred Maluma wa Njombe (Mawasiliano ya Jamii).

Hiyo ndiyo picha mpya ya uongozi wa TEC, viongozi wake wakitarajiwa kuendeleza mema mengi yaliyoachwa na uongozi uliopita


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.