Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mratibu Elimu adaiwa kuchukua madawati
Mratibu Elimu adaiwa kuchukua madawati
By Habari Tanzania | Published  07/16/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:
na Joseph Zablon

WAKATI Kamati ya Wazazi katika Shule ya Msingi Buguruni ‘A’, imepiga mbiu ya kutaka wazazi kuchanga sh 3,000 kila mmoja kwa ajili ya madawati, Mratibu wa Elimu wa Kata hiyo, Paulina Nyaki, anadaiwa kutoweka na madawati 11 yenye thamani ya sh 440,000; mali ya shule hiyo.

Habari zilizopatikana zinasema mratibu huyo alichukua madawati hayo Desemba 9, 2003 na hajayarudisha. Kila dawati linagharimu sh 40,000.

Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Khadija Telela, na Mratibu huyo, hawana maelezo ya wazi kuhusu madawati hayo.

Anadaiwa kuchukua madawati hayo baada ya kueleza kwamba alikubaliwa na Mwalimu Telela.

Tanzania Daima ina ‘memo’ inayoonyesha mwalimu huyo akikubali madawati hayo yachukuliwe na mratibu.

Mlinzi wa shule hiyo alimwandikia barua Ofisa Elimu wa Wilaya, Juni 19, mwaka huu, kuelezea suala hilo, lakini hajapata jibu.

“Katika kikao cha wazazi hivi karibuni wamewataka wazazi kuchanga sh 3,000 kwa kila mtoto kwa ajili ya ununuzi wa madawati, haya mengine yako wapi?” alihoji mlinzi huyo.

Nyaki, alikiri kuchukua madawati hayo, lakini alisema hakumbuki iwapo yaliisharudishwa au la.

“Kwa kweli nilichukua, ilikuwa kwa shughuli yangu binafsi, niliwaagiza watu wayarudishe, lakini sina hakika kama walifanya hivyo,” alisema.

Aliongeza: “Nipe muda nifuatilie, lakini nakumbuka niliagiza yarudishwe, ngoja nitakupigia kukufahamisha.”


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.