Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Kina Zombe kusomewa maelezo ya awali ya mashahidi Julai 27
Kina Zombe kusomewa maelezo ya awali ya mashahidi Julai 27
By Habari Tanzania | Published  07/15/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Na Njumai Ngota na Ester Bulaya
 
MAHAKAMA ya Kisutu Dar es Salaam, Julai 27, mwaka huu, itaanza kusoma maelezo ya awali ya mashahidi, baada ya washitakiwa katika kesi inayomkabili Kamanda wa zamani wa Polisi Mkoa wa Rukwa Kamishna Msaidizi wa Polisi Abdallah Zombe (52) na wenzake 11, kumaliza kuandika maelezo ya nyongeza.
 
Wakili wa Serikali William Magoma, akisaidiana na Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Charles Kenyela, walidai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi Sivangilwa Mwangesi, kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na wapo tayari kusoma maelezo ya mashahidi yatakayotumika Mahakama Kuu.
 
Mbali na kukamilika kwa upelelezi huo, Magoma alidai kuwa washitakiwa hao ukiondoa Zombe, tayari wamekwishaandika maelezo hayo ya nyongeza na kwamba wako tayari kusomewa.
 
Juni 29, mwaka huu washitakiwa hao wakiongozwa na mshitakiwa wa tatu katika kesi hiyo, Ahmed Makelle ambaye ni Mrakibu Msaidizi wa Polisi waliiomba Mahakama iwape nafasi ya kuandika maelezo ya ziada mbali ya yale waliyoyatoa Polisi wakati wakihojiwa.
 
Katika kesi hiyo ambayo Zombe ni mshitakiwa wa kwanza, washitakiwa wengine ni Mrakibu wa Polisi Christopher Bageni, Konstebo Jane Andrew.
 
Wengine ni Koplo Nyangekera Moris, Koplo Emmanuel Mabula, E. 6712 Felix Cedrick, Konstebo Michael, D. 2300 Abeneth na Koplo Rajabu.
 
Washitakiwa wote kwa pamoja wanashitakiwa kwa mashitaka manne ya mauaji wanayodaiwa kuyafanya Januari 14, mwaka huu, kwenye msitu wa Pande, uliopo Mbezi Loius, Dar es Salaam.
 
Kwenye shitaka la kwanza wanadaiwa kumuua Ephrahimu Chigumbi, shitaka la pili ni mauaji ya Sabinus Chigumbi, shitaka la tatu mauaji ya Juma Ndugu na shitaka la nne ni mauaji Mathias Lunkombe.
 
Washitakiwa walirudishwa rumande hadi Julai 27, mwaka huu, wakati maelezo hayo yatakapoanza kusomwa.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.