Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Kibondo yazindua jeshi jipya maalumu la mgambo
Kibondo yazindua jeshi jipya maalumu la mgambo
By Prosper Kwigize | Published  07/14/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Mwandishi wa HabariTanzania.com, Kibondo

Serikali wilayani Kibondo wiki hii imezindua jeshi maalumu la ulinzi katika ngazi za vitongozji ili kukabiliana na vitendo vya uharifu, umiliki na utumiaji wa siraha haramu katika vijiji.

Katika kukamilisha hilo Jeshi la ulinzi wa mgambo limetakiwa kuhakikisha linapambana kikamilifu na uzagaaji na uvutaji bangi katika vitongoji vyao ili kuwanusuru vijana na madhara yatokanayo na utumiaji w zao hilo.

Agizo hilo limetolewa leo na mkuu wa wilaya ya Kibondo luteni kanali John Mzurikwao wakati akihutubia kilele cha mafunzo maalum ya mgambo kwa wanamgambo wateule kutoka katika vitongoji takribani 800 wilayani humo.

Luteni kanali Mzurikwao amesema pamoja na kazi nyingine wanamgambo hao wanapaswa kuhakikisha bidhaa haramu ikiwemo pombe haramu ya moshi maarufu kama gongo inatokomezwa.

Ametoa siku tisini kuanzia july 14 hadi October 14 jeshi la mgambo kwa kushirikiana na viongozi wa serikali za mitaa kuhakikisha hakuna wakorogaji, wauzaji na wanywaji wa gongo, sambamba na wanaolima, kuuza au kuvuta bangi wawe wametokomezwa.

Aidha amewataka wanamgambo hao wapatao 1600, wawili kutoka katika kila kitongoji wilayani humo, kuunda vikundi vya ujasiriamali ili kupambana na umasikini miongoni mwao ambao ndio hupelekea kuwepo wa uarifu.

Awali mshauri wa mgambo wa mkoa wa Kigoma luteni Kanali Mapongo amewahimiza wanamgambo hao kuhakikisha wanafanya kazi zao katika vitongoji kwa kuzingatia maadili ya jeshi la mgambo.

Luteni kanali Mapongo amewahimiza wanamgambo hao kuwa makini na utumiaji wa madawa ya kulevya sambamba na kupambana na virusi vya ukimwi ili wawe mfano wa kuigwa na jamii njima.

Katika hafla hiyo wanamgambo wamekabidhiwa sare rasimi kama ishara ya kuanza kazi za ulinzi katika vitongoji na wilaya kwa ujumla.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.