Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Serikali kuu yaitaka halmashauri kibondo kushirikiana na jeshi la mgambo
Serikali kuu yaitaka halmashauri kibondo kushirikiana na jeshi la mgambo
By Prosper Kwigize | Published  07/14/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Mwandishi wa HabariTanzania.com, Kibondo
Agizo hilo limetolewa jana na mkuu wa wilaya ya Kibondo luteni kanali John Mzurikwao wakati akitoa maelekezo kwa wanamgambo na viongozi wa serikali za mitaa baada ya mafunzo ya ulinzi na usalama.
 
Luteni kanali Mzurikwao amesema shughuli za maendeleo zinaoendeshwa na halmashauri ya wilaya chini ya serikali za mitaa hazitafanikiwa endapo hakutakuwa na ulinzi wa kutosha katika mitaa na vijiji.
 
Amemtaka mkurugenzi wa halimashauri ya wilaya kushirikiana na jeshi la polisi kuweka mkakati imara wa kulinda watu na mali zao ili miradi inayoendeshwa na halmashauri isikwamishwe na kukosekana kwa Amani.
 
Awali kamanda wa polisi wilayani Kibondo amewataka wanamgambo kushirikiana na askari  polisi kuwafichua wahalifu na kuwafikisha katika vyombo vya sheria na ameonya juu ya kujichukulia sheria mikononi.
 
Jumla ya wanamgambo wapatao 140 kati ya 1600 wanaounda jeshi la mgambo la wilaya wameshiriki mafunzo maalumu ya wiki nne na kupewa sare rasimi za mgambo zilizofadhiliwa na mpango wa mendeleo wa umoja wa mataifa UNDP.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  3. Is Tanzania a safe place to invest?
  4. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
  5. Nitaendelea kugombea nafasi za kisiasa- Balozi Karume
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Linda Garner
  4. Nthelezi Nesaa
  5. Marshy Abdu
  6. Prosper Kwigize
  7. Salehe Mmoro
  8. Ramadhan Semtawa
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.