Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mishahara juu
Mishahara juu
By Habari Tanzania | Published  07/14/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:
Ansbert Ngurumo na Martha Mtangoo, Dodoma

SERIKALI imepandisha mishahara kwa watumishi wake, huku ikiwapa donge nono watumishi wa taaluma katika fani zote na walio katika vyombo vya ulinzi na usalama.

Hata hivyo, haikuweka bayana kima cha chini cha kipato cha watumishi hao.

Akiwasilisha bajeti yake bungeni jana, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hawa Ghasia, alisema ongezeko la mishahara litakuwa kati ya asilimia 15.9 na asilimia 50.

Alisema ongezeko hilo ni mojawapo ya jitihada za serikali za kuboresha masilahi ya watumishi wake, kwa kuzingatia Sera ya Muda wa Kati ya Malipo ya Mishahara.  

Usiri wa serikali katika kuongeza kiwango cha mishahara umewaudhi wapinzani, ambao wameitaka serikali itamke wazi ongezeko hilo.  

Walitaka pia serikali iainishe na kuonyesha kiasi kilichotengwa kwa ajili ya ajira mpya katika sekta za afya, elimu, maji na nyinginezo.  

Hoja ya upinzani iliwasilishwa na Waziri Kivuli wa Wizara hiyo, Shoka Hamis Juma, ambaye pia ni msemaji wa masuala ya Utawala Bora na Siasa na Uhusiano wa Jamii.  

Wapinzani walitaka serikali iweke mkazo wa pekee katika kuboresha masilahi ya watumishi wenye taaluma kulingana na thamani ya mchango wao kwa taifa.  

“Ni aibu kwa viongozi wetu na watu maarufu nchini kwenda kutibiwa nje, ili kuwafuata madaktari bingwa wakati inawezekana kufanyika hapa hapa nchini, tutambue kuwa wengi wa madaktari tunaowafuata huko Afrika Kusini na Nairobi ni Watanzania tuliowasomesha kwa kodi zetu,” alisema Juma.  

Katika hotuba yake ya bajeti, Waziri Ghasia alisema serikali imetenga sh milioni 1,003,882 kugharimia mishahara, ajira mpya na upandishaji vyeo kwa watumishi wa umma.  

“Kiwango hiki ni sawa na ongezeko la sh milioni 321,985, pia ni sawa na ongezeko la asilimia 47.22, ikilinganishwa na kiwango cha sh milioni 681,897 zilizotengwa kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2006/2006,” alisema Ghasia.

Nyongeza hiyo, alisema, itasaidia kuongeza ajira mpya 24, 689, upandishaji vyeo kwa watumishi wenye utendaji mzuri na kuongeza mishahara ya watumishi.

Waziri aliliomba Bunge liidhinishe sh 5,550,756,800 kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya Ikulu; sh 125,863,118,000 kwa ajili ya Ofisi ya Rais na Sekretarieti ya Baraza la Mawaziri; sh 58,430,104,500 kwa ajili ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma; sh 1,249,076,000 kwa ajili ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma; na sh 8,069,314,000 kwa ajili ya Tume ya Utumishi wa Umma.

Bunge lilipitisha bajeti hiyo jana jioni


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.