Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  ’Waislamu wachague Mufti Mkuu wenyewe’
’Waislamu wachague Mufti Mkuu wenyewe’
By Habari Tanzania | Published  07/13/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa kambi ya upinzani, wamepinga utaratibu wa Rais wa Zanzibar kumteua Mufti Mkuu kwa madai kuwa, ni kinyume na Katiba ya Zanzibar.

Wawakilishi hao wamesema, badala yake waachiwe waumini wenyewe kuchagua mtu anayefaa kwa mujibu wa sifa na vigezo walivyojiwekea.

Walisema walipochangia bajeti ya Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais Katiba na Utawala Bora, kwa mwaka wa fedha wa 2006/07 kwenye kikao cha Baraza la Wawakilishi kinachoendelea mjini hapa.

Mwakilishi wa jimbo la Chambani (CUF), Bw. Abbas Juma Muhunzi, alisema kama serikali inatetea utaratibu huo, basi hata viongozi wa Makanisa wakiwemo Maaskofu, wateuliwe na Rais.

Alisema ni jambo la kushangaza kuona Mufti wa Zanzibar anateuliwa na Rais wa Zanzibar, wakati Katiba imeweka wazi kwamba, serikali haina dini.

’’Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanini Mufti anachaguliwa na Rais, mbona Maaskofu hawachaguliwi na Rais, wakati huo huo tunaambiwa serikali haina dini,’’ alihoji Mwakilishi huyo.

Kwa mujibu wa sheria, Mufti anapaswa kupatiwa gari na mafuta kutoka serikalini kwa ajili ya shughuli zake.

Aidha, Mwakilishi huyo alisema, Katibu wa Mufti Zanzibar, Sheikh Fadhil Soraga, amekuwa akifanya kazi kwa jazba za kisiasa na kuishabikia CCM.

Alisema kiongozi huyo anatembea na kanuni za CCM katika semina za dini na ingekuwa jambo la busara akatafuta jimbo la uchaguzi kwa vile vitendo vyake vinasababisha mgawanyiko miongoni mwa waumini.

Naye Waziri Kivuli wa Wizara ya Nchi Katiba na Utawala Bora, Bw. Haji Faki Shaali (CUF), alisema ni vyema Mufti akateuliwa na Baraza la Maulamaa Zanzibar ili aweze kuwajibika kwao badala ya kuwajibika kwa Rais.

’’Uteuzi wa Mufti unaonekana kuwa na kasoro kwa vile anateuliwa na Rais jambo ambalo siyo sahihi,’’ alisema Bw. Haji Faki Shaali.
Akiwasilisha bajeti yake, Waziri wa Wizara hiyo, Bw. Ramadhan Abdallah Shaaban, alisema ofisi ya Mufti ilifanya kazi nzuri katika uchaguzi mkuu uliopita kwa kuhubiri amani na utulivu kwa kupitia kamati ya pamoja ya viongozi wa dini.

Alisema kamati hiyo iliwaelimisha wanasiasa na wananchi juu ya kuzingatia amani na umoja katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu.

Aidha, alisema ofisi ya Mufti iliweza kufanikisha utoaji taaluma kwa viongozi wa dini pamoja na waumini wao katika kupambana na maradhi dhidi ya janga la Ukimwi.

Waziri Shaaban aliliomba Baraza la Wawakilishi kuiidhinishia Ofisi ya Mufti Sh. milioni 98.6 kwa kazi za kawaida na Sh. milioni 58.9 kwa kazi za maendeleo.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.