Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Ndege ya UN yawaka moto
Ndege ya UN yawaka moto
By Habari Tanzania | Published  07/13/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Ndege ya kubeba mizigo inayomilikiwa na Umoja wa Mataifa (UN), ikiwa na askari watano, imeanguka na kuwaka moto mkoani Kigoma. Ilidondoka wakati ikijaribu kutua katika Uwanja wa Ndege wa mjini Kigoma.

Hata hivyo, askari wote, walinusurika kifo baada ya kuruka kutoka ndani ya ndege hiyo, kwa kutumia miavuli.

Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Kigoma, Bw. Elipid Tesha, alisema ndege hiyo ilikuwa ikitoka mjini Bunia katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuja mjini hapa.

Bw Tesha alisema baada ya askari hao kubaini hatari katika ndege hiyo, yenye namba UN 822, C 130 iliyotengenezwa nchini Urusi, waliamua kuruka kwa kutumia miavuli ili kuokoa maisha yao, huku wakiiacha ikiendelea kuwaka moto.

Alisema ajali hiyo ilitokea jana saa 10:00 jioni.
Bw Tesha alifafanua kuwa, ndege hiyo ina uwezo wa kubeba tani 30 za mizigo.

Lakini wakati wa tukio hilo, haikuwa imebeba mizigo.
Alisema baada ya ndege hiyo kuanguka, iliteketea kabisa kwa moto, baada ya juhudi za kutaka kuuzima kushindikana.

Kwa mujibu wa Meneja huyo, ndege hiyo ilikuwa inakuja Kigoma kufuata chakula na matunda kupeleka Bunia, DRC.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.