Majeshi ya umoja wa mataifa ya kulinda Amani katika nchi za afrika ya kati leo yamenusurika kupoteza maisha baada ya ndege lao la kijeshi kuanguka chini na kuteketea kwa moto muda mfupi kabla ya kutua mkoani Kigoma.
Ajali hiyo mbaya imetokea leo jumatano majira saa tisa na dakika thelathini na nne alasiri ikihusisha Ndege ya jeshi hilo iliyokuwa imebeba askari watano ambayo imeanguka na kuteketea kwa moto wakati ikijaribu kutua katika uwanja wa ndege wa mjini Kigoma ikitokea Congo-DRC
Akihojiwa na mtandao wa Habari Tanzania.Com akiwa katika eneo la tukio dakika chache mara baada ya ajali kutokea mfanyakazi wa uwanja wa ndege Bw.Shukuru Nziku amesema kuwa askari wote watano waliokuwemo ndani ya ndege hiyo walifanikiwa kuruka kwa kutumia miamvuli kabla ya ndege haijatua chini na kuwaka
Hata hivyo amesema akiwa anaendelea kuwasiliana na ndege hiyo ghafla mawasiliano yalikatika japo kuwa amesema kuwa ni mapema kueleza chanzo cha ajali hiyo.
Hata hivyo kwamujibu wa mfanyakazi huyo wa uwanja wa ndege mjini Kigoma Shukuru Nziku ndege hiyo imewaka moto na kuteketea kabisa huku askari wake wakielekea angani kwa miamvuli wakitumia mbinu za kijeshi.
Nae Bw.Nicolaus Busisi ambaye ni mfanyakazi wa shirika la world vision aliyekuwepo uwanjani hapo amesema kuwa wakiwa karibu na eneo la uwanja ghafla walishtukia ndege hiyo ikiwa imeanguka na kuwaka moto
Jeshi la polisi mkoani Kigoma halijatoa taarifa kamili kuhusiana na ajali hiyo ambayo yataugharimu umoja wa mataifa mabilioni ya pesa ili kurejesha mtandao wa mawasiliano baina ya nchi zenye migogoro za DRC na Burundi