Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Wanne kizimbani Z’bar kwa kuliibia Shirika la Umeme
Wanne kizimbani Z’bar kwa kuliibia Shirika la Umeme
By Habari Tanzania | Published  07/12/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Na Khatib Suleiman, Zanzibar
 
WAFANYAKAZI wanne wa shirika la umeme la Zanzibar, wakiwemo wanawake wawili, wamefikishwa katika mahakama tofauti wakikabiliwa na tuhuma za kulihujumu Shirika la Umeme pamoja na kuliibia zaidi ya sh. milioni 500.
 
Watuhumiwa walisomewa mashitaka tofauti ya wizi wa fedha ambapo Leluu Abdalla (48) anatuhumiwa kuiba sh. 25,385,693, wakati Ahmed Hamid Fatawi (38) anadaiwa kukwapua sh. 17,225,604.
 
Wengine ni Mohamed Abdalla Mohamed (43) aanayekabiliwa na tuhuma za kuliibia shirika sh. 491,667,986 na Fatma Bakari Omar anayedaiwa kuiba sh.2,636,875.
 
Watuhumiwa wote hao walishindwa kukamilisha masharti ya dhamana ambazo zipo wazi baada ya kutakiwa kulipa sh.milioni 10 kila mmoja, na kulipa sh. milioni moja fedha taslimu pamoja na kuwasilisha hati ya mali isiyohamishika.
 
Kesi zitatajwa tena Julai 25, mwaka huu. Hata hivyo haikuweza kufahamika mara moja kitakachowasibu washitakiwa wengine wa shirika hilo ambao walikuwa wakishikiliwa katika vituo tofauti vya Polisi tangu kukamatwa wiki iliyopita kufuatia ripoti ya Bodi ya Shirika la Umeme kuwataja kwamba wanahusika na upotevu mkubwa wa fedha.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.