BUNGE linaendelea na kikao chake leo ambapo Waziri wa Maji, Stephen Wassira, atasoma hotuba ya makadirio na matumizi ya wizara yake.
Hotuba hiyo ambayo itasomwa mara baada ya kipindi cha maswali na majibu, mjadala wake utaanza na kuhitimishwa kesho jioni.
Wiki iliyopita, Bunge lilipitisha makadirio na matumizi ya wizara ya Miundombinu na ile ya Kilimo, Chakula na Ushirika.
Bunge liliahirishwa Alhamisi kutokana na Ijumaa kuwa siku ya Sikukuu ya Sabasaba ambapo baadhi ya wabunge walishiriki kwenye maonyesho hayo mjini Dar es Salaam.