Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Baraza la Mawaziri la JK labariki programu ya kilimo
Baraza la Mawaziri la JK labariki programu ya kilimo
By Habari Tanzania | Published  07/8/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:
Na David Frank, Arusha

BARAZA la Mawaziri limepitisha Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo nchini; Rais Jakaya Kikwete, amethibitisha.

Akihutubia katika sherehe fupi za kuweka jiwe la msingi la upanuzi wa Kiwanda cha Uzalishaji Mbolea cha Minjingu, jana, Rais Kikwete alisema programu hiyo itaanza kutekelezwa mwaka huu wa fedha wa 2006/2007.

“Kwa ukubwa wake na kwa mpangilio wake wa kimkakati, ni kielelezo cha uthabiti wa dhamira ya serikali ya kuhakikisha kwamba mageuzi ya kilimo, ambayo tumekuwa tukiyaongelea kwa muda mrefu, sasa yanatokea.

“Utekelezaji wa programu hii ya miaka saba ni mwanzo wa safari yetu ndefu ya kuondokana na kilimo duni, chenye tija ndogo na mavuno kidogo.

“Katika kuifanikisha vizuri programu hiyo, tumepanga kutumia sehemu kubwa ya rasilimali katika ngazi ya wilaya na vijiji ambako ndiko waliko wakulima na ndiko kilimo kinapoendeshwa.

“Programu hii inaongeza rasilimali na uwezo wa kutekeleza Mipango ya Maendeleo ya Kilimo ya Wilaya ambayo ni sehemu ya Mipango ya Maendeleo ya Wilaya.

“Tumekuwa makini katika kuiandaa programu hii. Tumewashirikisha wadau karibu wote muhimu wa sekta ya kilimo nchini, tumetathmini gharama za utekelezaji wake, tumetafakari namna ya kupata rasilimali hizo na tumeanza mchakato wa kuzitafuta,” alisema.

Rais Kikwete alisema programu hiyo imekadiriwa kugharimu sh trilioni 2.492; lengo likiwa serikali yenyewe kuwa mchangiaji mkuu.

Hata hivyo, Rais Kikwete alisema wanakaribisha msaada kutoka kwa marafiki. Waliokwishaonyesha nia ya kusaidia ni Benki ya Dunia, Shirika la Misaada ya Ireland (Irish Aid), Serikali ya Japan, Umoja wa Nchi za Ulaya, na Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD).

Alisema madhumuni ya programu hiyo ni kuondoa umasikini wa Watanzania, mambo ambayo alisema yamekuwa yakihubiriwa kwa miaka mingi.

Katika programu hiyo, mambo ya msingi yaliyolengwa ni kuongeza matumizi ya maji katika kilimo; kuhimiza matumizi ya mbegu bora; kuongeza matumizi ya mbolea kurutubisha ardhi ya kilimo; kuboresha huduma za ugani kwa wakulima; kuimarisha masoko ya mazao ya mkulima; na kuboresha miundombinu na huduma nyingine muhimu zitakazosaidia kilimo kukua.

Rais Kikwete alisema ili kukifanya kilimo kiwe cha kisasa, makosa yaliyofanywa nyuma sharti yaepukwe.

Alisema kilimo kuwa uti wa mgongo pekee hakutoshi, bali kinapaswa kuboreshwa kwa kutumia pembejeo.

Rais aliipongeza Kampuni ya Minjingu Mines and Fertilizer Limited kwa uamuzi wake wa kuwekeza katika mradi huo.

Alisema kuwapo kwa kiwanda hicho ni moja ya kutimia kwa ndoto zake, tangu akiwa Naibu Waziri wa Maji, Nishati na Madini, na baadaye Nishati na Madini


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.