Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mawaziri wawili matatani
Mawaziri wawili matatani
By Habari Tanzania | Published  07/7/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Mwandishi Wetu

MAWAZIRI wawili katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano, wanadaiwa kumkwamisha mwekezaji mzalendo aliyepewa leseni ya kuchimba madini wilayani Ulanga, Morogoro.

Wanaotajwa kuhusika na mpango huo ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Celina Kombani; na Waziri wa Mipango, Uchumi na Uwezeshaji, Dk. Juma Ngasongwa.

Mwekezaji huyo mzalendo, anadai kukwamishwa kuwekeza kwenye uchimbaji madini wilayani humo, licha ya kupewa leseni halali kutoka mamlaka zinazohusika.

Wilaya ya Ulanga ina majimbo mawili ya uchaguzi - Ulanga Mashariki (Kombani), na Ulanga Magharibi (Juma Ngasongwa).

Mchimbaji huyo wa madini amelalamika kwamba viongozi hao, kwa kutumia nafasi zao za ubunge, wamehamasisha wananchi wamzuie kuchimba madini katika eneo hilo.

“Nina leseni halali ya kuchimba madini eneo la Ipanko, lakini nimezuiwa na wananchi wanaohamasishwa na mawaziri hao wawili.

“Wanasema siwezi kuchimba madini Ipanko, labda wanionyeshe eneo jingine, lakini siwezi kwenda eneo jingine kwa sababu leseni yangu imenielekeza eneo hilo ambalo nimeshalifanyia utafiti,” alisema.

Mwekezaji mwingine mzalendo alisema ni jambo la hatari kuona kuwa viongozi wakuu wanashiriki kuwahamasisha wananchi kuwakataa wachimbaji wazalendo.

“Hii ni kampuni ya wazalendo, ni ya Watanzania, kwa nini tuzuiwe? Kwani wageni ndio wenye haki ya kutetewa na viongozi?” alihoji mchimbaji huyo.

Kombani jana alizungumza na Tanzania Daima kwa simu kuhusu tuhuma hizo, na kusema hajui lolote kuhusu madai hayo.

“Sina habari, na si kweli kuwa mimi na waziri mwenzangu tunawahamasisha wananchi kupinga kampuni hiyo.

“Siwajui kabisa, Ipanko kuna wawekezaji wengi wanaokuja, nadhani kuna jambo jingine zito zaidi ya hilo, sijawahi kuonana na hao wanaolalamika.

“Siwezi kuhamasisha wananchi wampinge mwekezaji, tena mwekezaji wa ndani, siwezi,” alisema Kombani.

Pamoja na maelezo hayo ya Kombani, uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima umebaini kuwa kuna kundi la vijana wanaohamasishwa kumzuia mwekezaji huyo mzalendo


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.