MMOJA wa viongozi wa kundi la wanachama wa Yanga, maarufu kama ‘Yanga Family’, Hashim Lundenga amempongeza Mkurugenzi wa Quality Group, Yussuf Manji, kwa mikakati yake ya kuiboresha timu ya Yanga akiwa na mipango ya kutaka kuleta kocha mpya.
Akizungumza jana Dar es Salaam, Lundenga alisema kwamba wanachama na viongozi wa Yanga hawana budi kumpa ushirikiano Manji ili kuiweka timu hiyo katika mikakati ya kusaka ubingwa katika ngazi ya kimataifa.
“Nimefurahishwa sana kusikia Manji analeta Kocha, ni jambo zuri sana, Yanga imecchukua ubingwa mara nyingi hapa nchini kuizidi timu ya Simba na timu nyingine, hivyo tuitumie nafasi hii katika kujiimarisha kisoka,” alisema Lundenga.
Alisema kwamba kwa hilo la kumleta kocha, mdhamini huyo ameona mbali na kwamba kundi la wanachama wa Yanga Family litaendelea na harakati zake za kuleta maendeleo, na kamwe halitabweteka na udhamini wa Manji.