Wakazi wa wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma wamelalamikia kupanda kwa bei ya Nyama pamoja na sigara.
Wakiongea na mtandao wa HabariTanzania.com baadhi ya wakazi wa mji wa Kibondo wamebainisha kuwa bei ya nyama imepanda kwa asilimia 70 ambapo kilo moja ya nyama inauzwa shilingi 2000 hadi 2500.
Aidha wameeleza kuwa bei ya sigara nayo imepanda kutoka shilingi 50 hadi 80 hali ambayo inasababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa bidhaa hiyo.
Akiongea na wanadishi wa habari mmoja wa wamiliki wa maduka ya kuuzia nyama mjini humo Bw. Bangirimana Emanuel amesema kupanda kwa bei hiyo kumetokana na kupanda kwa bei ya ng’ombe minadani.
Bw. Emanuel amefafanua kuwa wilaya ya Kibondo haina Ng’ombe wa kutosha kwa ajili ya nyama na badala yake wafanyabiashara hununua ng’ombe hao kutoka wilaya Bukombe na Geita.
Amebainisha kuwa bei ya ng’ombe kwa sasa mnadani ni shilingi laki mbili hadi tatu badala ya shilingi laki moja na nusu bei ya awali.