Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Kikwete, Lowassa wanayajua haya?
Kikwete, Lowassa wanayajua haya?
By Habari Tanzania | Published  07/4/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Mwandishi Wetu

WAFANYABIASHARA wakubwa wa mafuta ya kula, wanafanya kila linalowezekana, ikiwa ni pamoja na kuwarubuni baadhi ya viongozi serikalini ili kuhakikisha kuwa wanafutiwa ushuru wa asilimia 10 kwenye mafuta ghafi wanayoingiza nchini.

Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima, umebaini kuwa baada ya serikali kuweka ushuru wa asilimia 10 kutoka sifuri, wafanyabiashara hao ‘hawalali’.

Wamefanikiwa kuwaona viongozi kadhaa, wakiwamo mawaziri ili wawasaidie kuhakikisha kuwa ushuru huo unafutwa na kubaki sifuri kama ilivyokuwa awali.

Wafanyabiashara hao wanatetewa na mtandao mpana wa baadhi ya viongozi, jambo ambalo limekuwa likitiliwa shaka na wafuatiaji wa uadilifu wa viongozi nchini.

Jana na leo, baadhi ya wafanyabiashara hao wapo mjini Dodoma, wakifanya mikutano ya siri na baadhi ya viongozi wanaodhani kuwa wanaweza kuwasaidia kufutwa kwa ushuru huo.

Siku moja kabla ya Bunge kupitisha bajeti ya Wizara ya Fedha, walifika Dodoma kwa nia ya ‘kumlegeza’ Waziri wa Fedha, Zakhia Meghji, ili awafutie ushuru huo, lakini waligonga mwamba.

Kuna habari kwamba Meghji alikataa kukutana nao, badala yake walikutana na waziri mwingine (jina tunalo) na kufanya mazungumzo kwa lengo la kunusuru mambo.

Hata hivyo, Zakhia akijibu hoja za wabunge, mwishoni kabisa, kwa majibu yake, alisisitiza kuwa ushuru huo lazima ulipwe.

Kauli ya Meghji ilionekana kuwa na nguvu kwa vile hakuna mbunge aliyepinga uamuzi huo murua wa serikali, lakini kuna habari kwamba wafanyabiashara walijipanga wakijua wapi wanaweza kupenyeza suala lao.

Katika kuhakikisha kuwa suala hilo wanalivalia njuga, kuna habari kwamba moja ya wizara imeandaa mkutano utakaofanyika Julai 11, mwaka huu mjini Dar es Salaam, au Dodoma.

Chanzo cha habari kimesema mkutano huo unafanywa kwa kivuli cha wadau wa mafuta, ingawa wakulima wadogo wa Tanzania, ambao soko na uchumi wao umeyumbishwa na mafuta kutoka nje, hawashirikishwi.

“Mkutano umeandaliwa, wanasema ni wa wadau wa mafuta, lakini hakuna mkulima mdogo aliyealikwa. Wanataka wakae, wajadiliane, kisha watoe taarifa kuonyesha kuwa wadau wanataka ushuru wa asilimia 10 ufutwe.

“Huu ni ujanja unaofanywa sasa, Rais na Waziri Mkuu wanapaswa wajue hili suala, Waziri wa Fedha tunamwamini, amejitahidi sana kukwepa suala hili, lakini wafanyabiashara hawa wana mbinu nyingi,” kilisema chanzo chetu.

Kwa miaka mingi sasa, serikali imekuwa ikikosa mabilioni ya shilingi kutokana na wafanyabiashara ya mafuta ya kula wanaoingiza kile wanachokiita kuwa ni malighafi kutoka Malaysia na nchi nyingine za Asia.

Hata hivyo, imebainika kuwa kinachoingizwa nchini si malighafi, bali ni mafuta yanayokuwa yameshasafishwa, lakini yanawekewa kemikali ili yaonekane kuwa ni machafu.

Wataalamu wanasema kuwa mawese hayawezi kubaki katika hali yake ya kawaida, saa 24 baada ya kusindikwa kama malighafi.

Kutokana na mafuta hayo kuingizwa nchini bila kulipiwa ushuru, wakulima wadogo wa Tanzania wameumia.

Wameumia kutokana na viwanda vya ndani ambavyo hutegemea mbegu kama za pamba, karanga na alizeti, kushindwa kuhimili ushindani usio wa haki.

Akifunga mjadala wa hoja yake bungeni, Meghji alisifu uamuzi wa serikali, kwa kusema siku chache baada ya kuweka ushuru kwa mawese kutoka nje, bei ya alizeti ilipanda kutoka sh 170 hadi sh zaidi ya 200 kwa kilo


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.