MAONYESHO ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam, yamedorora kutokana na wananchi wachache kujitokeza.
Kudorora kwa maonyesho hayo kulionekana dhahiri juzi na jana, kwani licha ya kuwa siku za mapumziko, wananchi wachache ndio waliotembelea maonyesho hayo.
Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima umebaini kuwa kudorora kwa maonyesho hayo kumechangiwa na kiingilio kuwa kikubwa.
Mwaka huu watu wazima wanalipa sh 2,000 na watoto sh 1,000, kiwango ambacho kinadaiwa kuchangia kuwapo mahudhurio hafifu, tofauti na miaka iliyopita.
Baadhi ya wananchi waliozungumza na Tanzania Daima, walisema viwango vya kuingia kwenye maonyesho hayo ni kikwazo kwa wengi.
“Wapo wanaokuja Sabasaba kutafuta bidhaa, ingawa kundi la aina hii ni wachache, lakini lipo kundi kubwa linalokuja Sabasaba kwa ajili ya kutembea na familia.
Ukipanda daladala, nauli juu, kuingia getini, bei juu, ndiyo maana wanaojitokeza ni wachache,” alisema Fadhili Abdallah.
Kwa upande wa wafanyabiashara, baadhi yao wamelalamikia kodi kubwa tofauti na miaka iliyopita.
Mmoja wa wafanyabiashara ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe, alisema mwaka huu haoni faida ya kushiriki maonyesho hayo, kwani wanunuzi ni wachache na kodi wanayolipa ni kubwa.
Mfanyabiashara huyo aliitaka Bodi ya Biashara ya Nje (BET), ipunguze kodi na kiingilio siku zilizobaki na siku ya kilele, ili wananchi wengi waingie na kufanya manunuzi ya bidhaa