Habari Tanzania - http://www.habaritanzania.com
Majambazi Wavamia Kambi Ya Wakimbizi Na Kupora Mali Na Fedha
http://www.habaritanzania.com/articles/432/1/Majambazi-Wavamia-Kambi-Ya-Wakimbizi-Na-Kupora-Mali-Na-Fedha
By Prosper Kwigize
Published on 07/3/2006
 

Watu wanaodhaniwa kuwa majambazi wamevamia na kupora fedha tasilimu shilingi laki tatu na nusu pamoja na vitu mbalimbali katika kambi ya Kanemba wilayani Kibondo.


Kibondo

Watu wanaodhaniwa kuwa majambazi wamevamia na kupora fedha tasilimu shilingi laki tatu na nusu pamoja na vitu mbalimbali katika kambi ya Kanemba wilayani Kibondo.

Mratibu msaidizi wa Polisi wilayani humo Japheth Kibona amesema kuwa tukio hilo limetokea jana majira ya saa mbili na nusu kwa Bw Barakanfitie Adelino anaeishi Block I kambini humo.

Vitu vingine vilivyoibwa ni pamoja na Radio mbili zenye thamani ya shilingi elfu 22, shuka mbili, suruali mbili aina ya Jinzi, viatu pea mbili na Blanket.

Katika tukio hilo hakuna mtu aliyejeruhiwa kwani Bw Barakanfitie na mkewe walifanikiwa kukimbia na kuwaacha majambazi hayo yakiendelea na uporaji.

Habari kutoka kambini humo zinaeleza kuwa tukio hilo la uporaji lilifanyika katika kipindi cha nusu saa huku majambazi hayo yakiendelea kurusha risasi hewani.

Mrakibu Msaidizi wa polisi wilayani Kibondo amesema hadi sasa hakuna watu wanoshikiliwa kutokana na tukio hilo lakini akabainisha kuwa juhudi za kuwasaka watu hao zinaendelea.